NA KIJAKAZI ABDALLA, MAELEZO ZANZIBAR
NAIBU waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Tanzania Mhandisi Atashasta Nditiye amesema
kumeibuka uhalifu unaowezesha na upatikanaji kwa rahisi wa taarifa binafsi
ambazo huhatarisha maisha ya watu na mali zao.
Aliyasema hayo katika
mkutano wa kuwasilisha mapendekezo ya kutunga sheria ya kulinda taarifa binafsi
kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar uliofanyika katika hoteli ya Zanzibar
Ocean View Kilimani.
Alisema kuwa
kutokana na maendeleo ya Teknolojia ya habari bna mawasiliano (TEHAMA) kuna kiasi
kikubwa cha taarifa binafsi zinazokusanywa na kuhifadhiwa ambapo pamoja na
matumizi mazuri ya taarifa hizo pia wapo kuna matumizi mabaya yakiwemo uhalifu.
Alieleza kuwa ulinzi
wa taarifa hizo unahitajika ili kujenga misingi mizuri ya matumizi ya taarifa
binafsi katika jamii kunakopelekea uhitaji wa sheria ambayo zitazoweka muongozo
wa ukusanyaji, utunzaji na usambazaji wa taarifa hizo.
Alisema kuwa
teknojia imekuwa na inahitaji kuwa na sheria ambayo inayopendekeza itatumia
pande zote mbili ya jamuhuri ya muungano na machakato wake ulianza wa kutunga
sheria na vikao mbalimbali vimekuwa vikifanyika tangu mwaka 2009.
Mhandisi Nditiye
alisema kuwa misingi mikubwa ya kutungwa kwa sheria hiyo ni utekelezaji wa
Ibara ya 16 ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 na Ibara ya
15 ya Katiba ya Zanzibar ya 1984 na kwamba sheria hiyo inayopendekezwa ni ya
usalama wa mtandao kutokana na ukiukwaju wa teknolojia.
Nae Mwanasheria wa
sekta ya Mawasiliano Eunice Masigati amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi
zilizoathirika na uhalifu wa mitandao ikiwemo uhalifu unaotokana na matumizi
mabaya ya taarifa binafsi.
Hivyo alisema kwamba
usimamizi wa kisheria wa masuala yanayohusu udhibiti wa matumizi na ufikiaji wa
taarifa zilizopo kwenye mifumo ya kompyuta na mitandao kwa ujumla.
Aidha alisema kuwa
kulinda taarifa binafsi itahusu udhibiti wa namna ambavyo taarifa za mtu, kampuni
au serikali zinavyoweza kutumika kwa kuwa na umuhimu wa kutunga sheria ambayo
itapendekezwa kulinda taarifa binafsi.
Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Tanzania Dk. Atashasta Nditiye akitoa hotuba ya ufunguzi wa Semina ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuhusu Mapendekezo ya kutungwa kwa Sheria ya kulinda taarifa binafsi iliofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani mjini Unguja.
Mwanasheria Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano Tanzania Eunice Masigati akiwasilisha mada kuhusu Mapendekezo ya
kutungwa kwa Sheria ya kulinda taarifa binafsi katika semina ya Wajumbe wa
Baraa la Wawakilishi iliofanyika katika wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View
Kilimani mjini Unguja.
Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura Hamza Hassan Juma (aliesimama) akichangia mada katika Semina kuhusu mapendekezo ya kutungwa kwa Sheria ya kulinda taarifa binafsi ilioandaliwa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Tanzania iliofanyika katika hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani mjini Unguja.
Waziri wa Ujenzi
Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Balozi Ali Karume (kulia) akitolea ufafanuzi baadhi ya maswali
yalioulizwa katika Semina ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi
kuhusu Mapendekezo ya kutungwa kwa Sheria ya kulinda taarifa binafsi iliofanyika
katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani mjini Unguja.
Spika wa Baraza la wawakilishi Zanzibar Zubeir
Ali Maulid (katikati) akitoa maelezo katika semina ya siku moja kwa wajumbe wa
baraza la wawakilishi kuhusu sheria ya kulinda taarifa binafsi iliyoandaliwa
kwa pamoja na wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano ya Tanzania na wizara
ya ujenzi, mawasiliano, uchukuzi na mawasiliano Zanzibar. Kulia kwake ni Naibu Spika Mgeni Hassan Juma.
No comments:
Post a Comment