NA MWINYIMVUA
NZUKWI
Jeshi la polisi Mkoa
wa Mjini Magharibi Unguja, limewafikisha watuhumia 93 wa makossa mbali mbali ya
udhalilishaji wa kijinsia katika mahkama za mkoa huo ikiwemo ya Hassan Aboud
Talib maarufu ‘Kiringo’.
Kamanda wa polisi
mkoani humo Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Msaidizi Kamishna Hassan Nasssir Ali aliwaambia
waandishi wa habari ofisini kwake Mwembe madema wakati akitoa taarifa za
matukio mbali mbali yaliyotokea katika wiki iliyopita na kueleza kuwa hiyo ni
awamu ya tatu ya kundi la watuhumiwa hao kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Alisema jeshi hilo
bado linaendelea na mkakati wake wa kupunguza makossa hayo licha ya kushindwa
kuwapata watuhumiwa 39 kati yao ambao kutokana na kutowapata kwa wakati muafaka
na wengine kuruka dhamana walizowapatia.
Alifahamisha
kuwa jeshi la polisi litawachukulia hatua za kisheria wadhamini wa
watuhumiwa hao baada ya kukiuka masharti ya dhamana kwa kushindwa kuwarudisha
kituoni pale wanapohitajika.
“Polisi inapozuia
dhamana dhidi ya baadhi ya watuhumiwa huonekana kama inakiuka sheria au haki za
watuhumiwa lakini hapa tuna mifano ya kesi nyingi ambazo watuhumiwa hawadudi
kituoni baada ya kupewa dhaman ana kupelekea kushindwa kuanza kwa wakati kwa
kesi husika”, alieleza Kamanda Nassir.
Mapema asubuhi
mamia ya wananchi, wanaharakati na wanahabari walifunga kambi katika viunga vya
mahakama kuu ya Zanzibar kwa lengo la kumshuhudia ‘Kiringo’ akifikishwa
mahakamani kwa mara ya kwanza baada ya kukamatwa wiki iliyopita akituhumiwa
kumlawiti mtoto wa kiume wa miaka 14.
Hata hivyo kesi
hiyo inayovuta hisia za watu wengi ndani na nje ya Zanzibar inayosikilizwa na
hakimu Valentine Andrew imeahirishwa hadi kesho Februari 27 wakati hakimu huyo
atakapotoa hukumu juu ya ombi lililotolewa na wakili wa mtuhumiwa la kupatiwa
dhamana mteja wake ombi ambalo awali lilipingwa na upande wa jamhuri na kuzusha
mabishano ya kisheria kati ya pande mbili hizo.
Hassan Aboud Talib 'Kiringo' mmoja ya watuhumiwa wa kesi za udhalilishaji waliofikishwa mahakamani.
No comments:
Post a Comment