NA MWINYIMVUA NZUKWI
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud amewataka watendaji
wa taasisi za serikali na jeshi la polisi kufanya utafiti wa kina ili kubaini vyanzo vya vitendo vya udhalilishaji wa
kijinsia wa wanawake na watoto.
Akifungua mafunzo maalum ya siku kumi
Kwa watendaji wanaoshughulikia makosa ya udhalilishaji wa
kijinsia na ukatili wa watoto yaliyoandaliwa na jeshi la polisi, katika makao
makuu ya jeshi la polisi Zanzibar alisema endapo jeshi hilo litafanikiwa
kubaini chanzo na
viashiria vya matendo ya udhalilishaji itasaidia kupunguza kasi
ya matendo hayo yanayoharibu jina la nchi.
Alisema hatua zinazochukuliwa ili kudhibiti kasi ya vitendo
hivyo zitafanikiwa iwapo elimu ya kutambua viashiria vyake na kupelekea
kupungua na kudhibitiwa katika jamii.
“Wakati tukitafuta njia za kutambua viashiria vya matukio haya
ninawaomba muendeleze
Nidhamu na kufanya kazi hii kwa kuzingatia maadili, uzalendo na
uwajibikaji katika kutumia nafasi zenu za kutimiza malengo ya kupambana na
vitendo hivi pamoja na changamoto zinazowakabili”, alisema RC Ayoub.
Wakizungumza katika mafunzo hayo baadhi ya washiriki wa mafunzo
hayo wamesema changamoto wanazokumbana nazo wanaposhughulikia aina hiyo ya uhalifu
huo uchache wa elimu na ujuzi unaohusiana na masuala ya udhalilishaji kwa
wananchi.
Hata hivyo walisema tatizo la muhali miongoni mwa jamii
kunakopelekea jamii kumaliza kesi hizo mitaani jambo linalorudisha nyuma juhudi
za serikali na wadau mbali mbali katika kuondosha vitendo vya udhalilishaji kwa
wanawake na watoto.
Akizungumza katika mafunzo hayo Kamishna wa kamisheni ya polisi
jamii Tanzania, Kamishna Mussa Ali Mussa alisema jeshi la polisi halitamvumilia
askari yeyote atabainika kujihusisha na uharibifu wa kesi na ushahidi
unaohusiana na kesi hizo.
Aliongeza kuwa jeshi hilo limendaa mikakati mbali
mbali ukiwemo wa uundaji wa madawati ya jinsia ili kuhakikisha kesi
za udhalilishaji zinafanyiwa upelelezi wa kina na kuchukuliwa hatua za kisheri
na kuwataka watendeji hao kuwa karibu na jamii.
Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud akifungua
mafunzo kwa askari polisi na maafisa wa ustawi wa jamii kuhusiana na kudhibiti
vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia na watoto.
No comments:
Post a Comment