NA MWINYIMVUA NZUKWI
Rais
wa Zanzibar na Baraza la Mapindunzi na Mwenyekiti wa Baraza la Mapindunzi Dk. Ali
Mohamed Shein amewataka wafanyabiashara watakaopata nafasi ya kufanya biashara katika
jumba la Chawal (jumba la treni) kudumisha usafi ili liweze kutumika kwa muda mrefu.
Akihutubia
wananchi katika uzinduzi wa jengo hilo liliopo Darajani Mjini Unguja baada ya
kufanyiwa matengenezo makubwa, Dk. Shein amesema jengo hilo lina historia kubwa
hivyo kuimarishwa kwa usafi kutaongeza sifa ha haiba ya mji wa Zanzibar.
Amesema
uamuzi wa serikali kulifanyia matengenezo jumba hilo yaliyosimamiwa na mfuko wa
hifadhi ya jamii Zanzibar (ZSSF) Dk. Shein amesema umelaenga kuweka mazingira
mazuri ya ufanyaji biashara na kutunzwa historia ya jingo hilo ambalo ni sehemu
ya urithi wa kimataifa.
"Tulipoamua kulijenga upya jengo hili tulikuwa tunadhamira ya dhati ya kulinda na kuhifadhi historia ya nchi yetu katika masuala ya biashara bila ya kuathiri uhalisia wake na ndio maana kabla ya kuanza kujenga tulihakikisha tunazingatia maelekezo ya UNESCO", amesema.
Ameupongeza
uongozi na wafanyakazi wa wizara ya Fedha na Mipango, Mfuko wa hifadhi ya
jamii (ZSSF) na Mshauri mwelekezi wa mradi huo kwa kusimamia kikamilifu ujenzi wa jengo hilo uliotekelezwa na kampuni ya CRJE ya China kwa kufuata vigezo vilivyowekwa na shirika la kimataifa la sayansi na
utamaduni (UNESCO) na kusimamia uendeshaji.
"Kama tulivyotekeleza mradi huu, tutakeleza miradi mingine ukiwepo huu wa ujenzi wa maduka ya kisasa hapa Darajani mara baada ya kukamilisha taratibu zilizowekwa na UNESCO kwani eneo hilo lipo katika ukanda wa urithi wa kimataifa", amesema Dk. Shein.
Nae
Waziri wa Fedha na mipango Zanzibar Dk. Khalid Salum Mohammed amempongeza Rais Dk. Shein kwa kusimamia maelekezo yake kila mara yaliopelekea kupatikana kwa
mafanikio ya mfuko huo katika uwekezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo
nchini.
Amesema
katika kipindi cha miaka 20 ya uhai wa mfuko huo, umeweza kutekeleza miradi ya
ujenzi na uwekezaji kiuchumi iliyolenga kuiamarisha uwezo wa mfuko huo ili
kutoa huduma kwa wanachama wake.
Amaitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa
mnara wa kumbu kumbu ya mapinduzi, ujenzi wa viwanja vya kufurahishia watoto
vya Kariakoo mjini Unguja na Tibirinzi kisiwani Pemba, ujenzi wa nyumba za makaazi na
ukarabati wa jengo hilo na katika muda
mchache ujao ZSSF itaanza ujenzi wa maduka ya kisasa katika eneo la Michenzani.
Aidha
Dk. Khalid amewapongeza wafanyabiashara waliokuwa wakifanyabiashara na wakaazi wa jengo hilo kwa
kukubali kuhama ili kupisha ujenzi huo na kuwahakikishia kuwa serikali itaendelea kujenga
miundombinu rafiki ya kukuza biashara nchini ikiwa ni utekelezaji wa
ilani ya uchaguzi ya CCM na ahadi ra Rais alizozitoa wakatiki wa kampeni.
Mapema
akitoa taarifa kuhusu ujenzi huo, Mkurugenzi Mwedeshaji wa ZSSF Sabra Issa
Machano amesema ujenzi huo ulihusisha makampuni mbali mbali utasaidia kukuza
uchumi wa nchi kutokana na shughuli zitakazoendeshwa ndani ya jengo hilo pamoja
na kuwa kivutio cha utalii.
Amesema
ujenzi huo uliochukua miezi 20 hadi kukamilika kwake, umegharimu shilingi
bilioni 11.5 ambapo mbali ya milango ya 52 ya maduka, ndani ya jengo hilo
kutakuwa na nyumba 10 za makaazi, mgahawa, ukumbi wa mazoezi na vyumba vya
mashine za kielektroniki za kutolea fedha (ATM).
Akizungumzia
ujenzi huo Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud amemshukuru
rais wa Zanzibar kwa kusisitiza uadilifu miongoni mwa wafanyabiashara na
wasimamizi wa mradi huo ili uweze kuleta mafanikio.
Aidha
amemshukuru Dk. Shein kwa kuridhia kuendelea kuishi katika jengo hilo bila ya
malipo mmoja ya wakaazi wa awali wa jengo hilo bi. Zuwena ambae alikuwa mtu wa
mwisho kuhama katika jengo hilo kabla ya kukabidhiwa kwa mkandarasi kwa ajili
ya ujenzi.
Amesema
mama huyo licha ya kuwa na vielelezo vilivyomhalalisha kuishi katika jengo hilo
alivyopatiwa na serikali ya awamu ya kwanza iliyoongozwa na mzee abeid Amani karume,
mama huyo alikubali kupisha ujenzi huo na kupelekwa katika makaazi ya kulelea
wazee Sebleni.
"Mama huyu alikuwa ni miongoni mwa wakaazi wa jengo hili alieishi kwa muda mrefu zaidi ya mtu mwengine yeyote lakini alikubali kuondoka na kupisha ujenzi kufanyika lakini leo Mheshimiwa Rais ameagiza mama huyu apatiwe nyumba miongoni mwa nyumba zilizomo humu na aishi kwa muda wake wote bila ya malipo yeyote", amesema Ayoub.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (alievaa miwani) akihutubia wananchi wakati uzinduzi wa jengo la Chawl (Jumba la treni) baada ya kufanyiwa matengenezo makubwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF).
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Sabra Issa Machano (kulia) akitoa maelezo ya utekelezaji wa mradi wa matengenezo ya jengo la Chawl (Jumba la treni).
Muonekano wa jengo la Chawl (jumba la treni) baada ya kufanyiwa matengenezo makubwa na na kuzinduliwa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 ya
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF). PICHA KWA HISANI YA IDARA YA HABARI MAELEZO, ZANZIBAR.
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF). PICHA KWA HISANI YA IDARA YA HABARI MAELEZO, ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment