NA
MWINYIMVUA NZUKWI
MAKAMU
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema wakati Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar inazidi kuimarisha miundombinu ndani ya Sekta
ya Elimu, wanafunzi wanalazimika kujikita kutafuta elimu itakayowajengea maisha
ya furaha wao na familia zao.
Alisema
wanafunzi wakisoma kwa juhudi, maarifa na kufikia kiwango cha elimu ya juu ya
katika vyuo vikuu watakuwa na nafasi kubwa ya kujihakikishia za ajira
zilizozoweya kufanywa na Wataalamu wa Kigeni.
Balozi
Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Mwambe
katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo mapya ya skuli za
sekondari zinazojengwa kwa pamoja kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mshirika
wa Maendeleo Mfuko wa Kimataifa wa jumuiya ya maendeleo ya petroli ulimwenguni (OPEC).
Alisema
Taifa linahitaji wataalamu wake watakaotokana na wanafunzi ambao wanapaswa
kuweka malengo ya kusoma kwa bidii kwa lengo la kuwahudumia Wananchi kwa
kiwango cha uzalendo zaidi.
Balozi
Seif aliwahimiza watoto wa kike nchini kusoma kwa ziada ili zile kazi za
Kitaalamu zinazofanywa na Wanaume akatolea mfano za huduma za Afya wazifanye
wenyewe katika azma ya kulinda na kuheshima mila, sila, Tamaduni na hata imani
za Kidini.
Katika
kutilia mkazo nafasi ya mtoto wa kike kusoma kwa malengo Balozi
Seif ameagiza Wazazi wowote watakaohusika na kitendo cha
kuwaozesha Watoto wao wa Kike wakati wanasoma Uongozi wa Serikali ya
Mkoa usimamie katika kuona Vyombo vya Dola vinawachukulia hatua za Kisheria
mara moja Wazazi hao ikiwa ni pamoja na kuwaweka ndani.
“Jamii
inahitaji kuwa na Ewataalamu wa Kike ambao watahusika kushughulikia huduma
zinazofanywa na Wanaume Kitaalamu ambazo hazistahiki kutokana na Tamaduni na
Imani wa Kidini”. Alisisitiza Balozi Seif.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar alionya kwamba tabia hii inayoonekana kuendelea kwa
baadhi ya Mitaa Nchini inarejesha nyuma maendeleo ya Mtoto wa kike
aliyekandamizwa kwa muda mrefu kutokana na mfume Dume uliozoeleka kwa kipindi
kirefu kilichopita.
Alieleza
kwamba matukio hayo ni miongoni mwa matendo yanayoonyesha muendelezo
wa unyanyasaji wa Kijinsia uliomgubika Mtoto wa Kike unaopswa kuondolewa hivi
sasa kutokana na mabadiliko makubwa ya Sayansi na Teknolojia yaliyoanza
kumfunulia njia Mtoto wa Kike.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Wazazi na Wananchi wa Mwambe kutokana
na mwamko wao mkubwa wa kuwapelekea Skuli Watoto wao jambo ambalo linafaa
kuigwa na Wazazi wengine Nchini.
Alisema
Mikondo Mitatu ya Wanafunzi wanaoingia na kusoma kwenye Skuli ya Mwambe ni
ushahidi tosha wa Wazazi hao kutambua uhumihu wa Elimu licha ya Idadi kubwa ya
Wakaazi wake ambao Watoto wake walikuwa wakipenda sana kufanya kazi za U vuvi.
Mapema
Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdullah alisema ziara zake
za Majimbo Tisa akijumisha na maskuli yaliyombo kwenye Majimbo
hayo zimemthibitishia kukithiri kwa utoro kwenye Skuli nyingi za
Mkoa huo.
Mh.
Suleiman alisema bila ya Elimu hakuna Daktari, Mwalimu na hata Mhandisi, na
katika kutambua umuhimu huo Serikali ya Mkoa imeamua kwa makusudi Mzazi ambae
mtoto wake atatoroka Skuli atakamatwa na kushtakiwa kwa kosa la kumkosesha haki
ya Elimu Mtoto wake.
Mkuu
huyo wa Mkoa Kusini Pemba amewapongeza Swananchi wa Mwambe kwa
uwamuzi wao wa kuimarisha Ulinzi Shirikishi katika Shehia yao kitendo
kilicholeta faraja na Amani katika eneo hilo.
Mh.
Hemed alisema Kijiji cha Mwambe kilikuwa kikitajika kwa vitendo vya wizi wa
mazao na ulevi vilivyosababishwa na baadhi ya Vijana waliokosa muelekeo
kutokana na kukosa Taaluma ya Kimaisha.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar alikagua Maendeleo ya ujenzi wa Skuli za Sekondari
za Mwambe na Wara Ndugukitu na kuridhika na hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa
Skuli hizo.
Balozi
Seif aliwahimiza Wahandisi wa ujenzi wa Majengo hayo kuongeza jitihada ili
kuhakikisha kwamba Miradi hiyo inakamilika katika wakati uliowekwa pamoja na
kiwango cha hadhi inayokubalika ya kimajengo.
Mapema
asubuhi Balozi Seif alikagua Bara bara mpya inayojengwa kwa kiwango
cha Lami katika Kijiji cha Ole hadi Kianga inayokadiriwa kuwa na urefu wa
Kilomita 10.
Afisa
Mdhamini Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Hemed
Baucha alimueleza Balozi Seif kwamba kipande kilichobaki cha
Bara bara hiyo kimechelewa kumalizika kutokana na Nyumba Nne zilizolazimika
kuvunjwa kupisha ujenzi huo ambazo mwanzoni hazikuwamo.
Hata
hivyo Baucha alisema Wataalamu wa Wizara hiyo wameshafanya tathmini na
taratibu za malipo ya Fidia kwa Wananchi wanaohusika na Nyumba hizo zikamilike.
Balozi
Seif alipongeza Wataalamu wa Idara ya Utunzaji na Ujenzi wa Bara bara {UUB} kwa
kazi kubwa na nzuri waliyoifanya ambapo Serikali Kuu imeridhika na Taaluma
waliyonayo Wahandisi hao wazalendo.
Alisema
wakati Serikali inajitahidi kuangalia uwezekano wa kuwapatia vifaa zaidi vya
ujenzi Wahandisi wa Idara hiyo lakini bado wana dhima ya kuhakikisha kazi
wanazopewa wanazikamilisha kwa wakati muwafaka.
Wakati
huo huo Balozi Seif alifika Pagali kuangalia maendeleo ya ujenzi wa
Nyumba za Makaazi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Ujenzi
unaofanywa chini ya Wahandisi wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo
Zanzibar (KMKM).
Mshauri
Muelekezi Mkuu wa Ujenzi huo Mhandisi Ramadhan Mussa Bakari
alimueleza Balozi Seif kwamba Ujenzi huo ulioanza Rasmi Juni 23 mwaka huu
unaendelea vyema licha ya changamoto ya upatikanaji wa huduma za Maji.
Mhandisi
Ramadhan alisema ili kazi hiyo iendelee kama ilivyopangwa na kukusudiwa upo
umuhimu wa kuchimbwa Kisima ndani ya eneo hilo ili kuwa na uhakika wa
upatikanaji wa huduma hiyo muhimu.
Akikagua baadhi ya Majengo ya Nyumba hizo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliridhika na kiwango pamoja na uharaka wa Wahandisi hao wanaouendeleza na kujenga matumaini yake ya kumalizika Mradi huo kwa wakati uliopangwa.
PICHA NA MAELEZO YAKE
Wananchi wa Kijiji cha Mwambe kisiwani Pemba wakisimkiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi (hayupo pichani) baada ya kukagua Mradi wa Ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Mwambe inayojengwa kijijini hapo.
Mhandisi wa Ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Wara Ali Khamis Shaibu (alienyoosha mkono) akitoa maelezo kwa Balozi Seif (mwenye miwani) kuhusiana na maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Skuli hiyo unaokwenda kwa wakati uliopangwa. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri katika ofisi ya Makamu wa pili wa Rais Mihato Juma N'hunga.
Balozi Seif Ali Iddi (kushoto) akimchum mtoto Sulhia Ali wa Kijiji cha Mwambe huku Mama Mzazi wa mtoto huyo (kulia) akitabasamu mara baada ya kusalimiana na wananchi wa kijiji hicho kukagua maendeleo ya ujenzi wa skuli ya Sekondari ya Wara.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Maalim Abdulla Mzee Abdulla (wa pili kulia) akiteta jambo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwenye majengo ya Skuli Mpoya ya Sekondari inayojengwa katika Kijiji cha Wara Chake Chake Pemba.
Balozi
Seif akikagua baadhi ya Majengo ya nyumba za makaazi ya Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar zinazojengwa katika eneo la Pagali Wilaya ya Chake chake Pemba.
PICHA KWA HISANI YA OMPR.
No comments:
Post a Comment