NA MWINYIMVUA NZUKWI
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmuoud amesema
serikali ya Zanzibar itaendelea kuimarisha uhusiano baina yake na wawekezaji
kwa lengo la kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi na kuchochea maendeleo ya
jamii.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada wa vifaa vya skuli kwa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja Hassan Ali Kombo vilivyotolewa na Mfanyabiashara Said Nassir Nassor ‘Bopar’ kwa ajili ya wanafunzi wa skuli za Chaani Msingi na Sekondari, Ayoub amesema miongoni mwa faida zinazopatikana katika uwekezaji ni pamoja na kutumia sehemu ya uwekezaji wao kwa ajili ya jamii inayowazunguka.
“Serikali zetu zimekuwa zikipata faraja pale inapoona wawekezaji
wanaowekeza miradi yao nchini kwetu, wanasaidia harakati za maendeleo ya jamii pale
inapohitajika kwani hatua hii huleta mahusiano mazuri kati yao na husukuma
mbele kasi ya maendeleo ya wananchi pamoja na serikali yao”, alieleza Ayoub.
Aidha aliwaeleza wananchi na viongozi wa wilaya hiyo kuwa ataendelea kutimiza wajibu wake katika kuhudumia wananchi katika sekta zote za kimaendeleo bila ya kujali mipaka ya kiutawala na kuwataka kuunga mkono juhudi hizo kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika skuli ya
Chaani, Afisa wa elimu Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Mshamara Kombo amesema msaada
huo umekuja kwa katika wakati muafaka kwani utawasaidia walimu na wananfunzi wa
skuli hizo kutatua changamoto zinazozikabili skuli hizo na wananchi wa
maeneo hayo kuahidi kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa.
Katika hafla hiyo mfanyabiashara huyo alikabidhi misaada ya na mikoba
ya kubebea madaftari 500, Madawati 50 yenye uwezo wa kuchukua viti 100,
magodoro 20 kwa ajili ya wanafunzi wanaolala kambi wakati wa mitihani, seruni
na vitenge kwa wazee wa kiume na kike, vifaa vya michezo kwa ajiliya timu nne
za Chaani na vifaa vyengine vya kusomea ambavyo vyote vinakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud (kulia) akisalimiana na mmoja ya kina mama 30 kabla ya kukabidhi zawadi ya kitenge mara baada ya mkuu huyo kukabidhi vifaa vya skuli kwa wananfunzi wa skuli za Chaani Msingi na Sekondari. Kushoto alievaa kofia ni Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini 'A' Unguja Hassan Ali Kombo.
Mmoja ya wanafunzi wa skuli ya sekondari Chaani akionesha fedha alizopatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud kama msaada uliotolewa na Mfanyabiashara Said Nassir Nassor 'Bopar' kwa wanafunzi na skuli za Chaani msini na Sekondari.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud (kulia) akiagana kina mama wa shehia za Chaani mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kukabidhi vifaa vya skuli kwa wananfunzi wa skuli za Chaani Msingi na Sekondari na zawadi za nguo na vifaa vya michezo vilivyotolewa na mfanyabiashara Said Nassir Nassor 'Bopar'. Zaidi ya shilingi milioni 20 zinakadiriwa kutumika kwa ajili hiyo.
No comments:
Post a Comment