RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, amesema kuwa miongoni
mwa malengo ya Mapinduzi matukufu ya Januari 12, 1964 ni kufanya hali za maisha
ya Wazanzibari kuwa bora na ujenzi wa soko la Tibirinzi ni miongoni mwa malengo
hayo na sio kichocheo cha kubaguana kwa vyama, dini, jinsia au mahala mtu
anapotokea.
Dk. Shein amesisitiza kuwa jengo hilo jipya la soko
ni ukombozi kwa wakulima, wafanyabiashara, wafugaji, wavuvi na wajasiriamali
pamoja na wananchi wote kwa jumla kwa kuweza kuongeza kipato chao ili maisha
yao yaweze kuwa bora.
Rais Dk. Shein aliyasema hayo leo mara baada ya kulizindua soko jipya la Tibirinzi Chake Chake Pemba.
Rais Dk. Shein aliyasema hayo leo mara baada ya kulizindua soko jipya la Tibirinzi Chake Chake Pemba.
Dk. Shein alisemakuwa soko hilo si vyema
likahusishwa na masuala ya kisiasa kwani ni soko la watu wote wa vyama vyote,
dini zote na jinsia zote huku akiwataka wafanyabiashara watakaolitumia soko
hilo kuleta bidhaa zenye ubora zitakazolingana na hadhi ya soko hilo.
Alisema kuwa ujenzi wa soko hilo ni katika hatua za kutafsiri Mapinduzi ya mwaka 1964 kwa vitendo kwa kuwaletea wananchi maendeleo zaidi bila ya ubaguzi.
Alisema kuwa ujenzi wa soko hilo ni katika hatua za kutafsiri Mapinduzi ya mwaka 1964 kwa vitendo kwa kuwaletea wananchi maendeleo zaidi bila ya ubaguzi.
Alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
inatekeleza Sera mbali mbali zikiwemo zinazolenga kuinua kipato cha wananchi na
kupunguza umasikini.
Sambamba na hayo, Dk. Shein alisisitiza haja ya kulitunza na kulienzi soko hilo ikiwa ni pamoja na kudumisha usafi wa soko hilo kwani usafi ni jambo la lazima na halina mbadala.
Dk. Shein alitumia fursa hiyo kueleza mafanikio
sambamba na azma ya Mapinduzi Matukufu ya Januri 12, 1964 ambayo yamewakomboa
wananchi wa Zanzibar na kukata minyororo ya chuki na udhalimu sambamba na kunyanyaswa.
Alieleza madhumuni makubwa ya Mapinduzi ya Zanzibar
ni kuwa huru na hatua ambayo imepekea kupanga mambo bila ya kuingiliwa na mtu
na kuweza kuongoza nchi sambamba na kuandaa mipango ya muda mrefu na muda mfupi
na wakati.
Alieleza kuwa Zanzibar imepata maendeleo makubwa
katika kukuza uchumi wake ndani ya kipindi cha miaka 54 huku akieleza kuwa
mabadiliko makubwa ya kiuchumi, sera ya serikali maisha ya watu ambayo yote
hayo ni maendeleo.
“Leo naambiwa ndege zinazokuja Pemba hivi sasa
hazitoshi, meli hazitoshi watu wanasafiri kila leo hayo yote ni maendeleo na
kukua kwa uchumi.. jengo hilo ni lazima tulipe heshima yake” Alisema Dk. Shein.
Nae Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi
Hamad Rashid Mohammed alieleza kuwa kuna kila sababu ya kumuenzi na kumuombea
dua Rais Dk. Shein kwa maendeleo makubwa sambamba na juhudi anazozichukua
katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar.
Waziri Rashid alisema kuwa maendeleo yanayoonekana
na kwa mara ya kwanza katika historia wafanyakazi wameweza kulipwa mshahara
mara mbilili wanaopata, kuzalisha mpunga tani 39 elfu, kuwepo na mchele kutoka
Zanzibar pamoja na maendeleo mengineyo ikiwemo kuimarika kwa miundombinu.
Aliongeza kuwa Rais Dk. Shein kuwa Zanzibar imebaki salama kutokana na hekima yake na hakuna mpasuko na kumekuwa na amani kubwa kwani huwezi kupata maendeleo kama hakuna amani ya nchi.
Alieleza kuwa Dk. Shein ni kiongozi anaetaka kila
mmoja kutoa maamuzi na kumshirikisha kufanya hivyo na ndicho kilichomfanya Dk.
Shein kuweza kuwatumikia watu tena bila ya ubaguzi.
“Kina Mzee Karume wasingeweza kupindua nchi kama
wasingekuwa na nia nzuri… Mwenyezi Mungu peke yake ndie anaechagua kiongozi..
kwani katika mazingira haya nani angelijua kuwa Hamad Rashid angekuwa Waziri wa
Kilimo…unapomkuta kiongozi anajenga fitna kwa watu anajenga fitna kwa watu,
unapomkuta kiongozi anajenga makundi hata salamu alaykum haitikiii ni kweli
huyu mtu wa peponi?”,aliuliza Hamad Rashid.
Waziri Rashid aliwataka baadhi ya wananchi kisiwani
humo kuwacha siasa na badala yake washughulikie mambo ya msingi na yenye kuleta
maendeleo huku akieleza kuwa Serikali inalengo la kujenga masoko makubwa mawili
huko Malindi mjini Zanzibar na soko jengine litajengwa huko kiswani Pemba.
Mapema Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Maliasili,
Mifugo na Uvuvi Joseph Abdalla Meza alieleza kuwa soko hilo ni kati ya masoko
manne yaliojengwa Zanzibar kupitia Programu ya Miundombinu ya Masoko, Uongezaji
Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVAP) inayogharamiwa na Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB), Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) na
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aliongeza kuwa program hiyo inasimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi kwa Zanzibar na kueleza kuwa ujenzi wa soko hilo ulianza mwezi wa Aprili 2016 ambapo wazabuni 12 waliomba kufanya kazi hiyo na baada ya tathmini Kampuni ya ZECCON LIMITED ya Zanzibar ndiyo iliyoibuka mshindi na kupata tenda hiyo na kuingia mkataba wa ujenzi kwa gharama za TZS Milioni 972.2 ambapo kati ya hizo milioni 48.6 zimetolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Alisema akuwa soko hilo lina vibaraza 76
vitakavyokabidhiwa kwa wafanyabiashara ambapo soko hilo lina chumba cha baridi
kwa ajili ya kuhifadhia samaki na chumba maalum kilichotengwa kuwekewa mtambo
wa kutengenezea barafu ambao utawasaidia wavuvi kutumia barafu hizo wakati
wakiwa baharini.
CHANZO: Ikulu - Zanzibar
Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein akihutubia wananchi walihudhuria kushuhudia uzinduzi wa soko la kisasa liliopo Tibirinzi. Kulia ni Mhamoud Thabit Kombo waziri wa Afya Zanzibar.
Muonekano wa soko jipya la Tibirinzi baada ya kukamilika kwa ujenzi wake katika eneo la Chake chake mkoa wa Kusini Pemba,
No comments:
Post a Comment