NA MWINYIMVUA NZUKWI
Familia askari 10 wa Jeshi la Wananachi
wa Tanzania (JWTZ) waliouawa nchini Congo DRC mwishoni mwa mwaka uliopita zimeeleza
kuridhishwa na jitihada zinazochukuliwa na serikali za kuhakikisha zinawapatia
misaada ya hali na mali ili kukabiliana na changamoto mbali mbali baada ya kuondokewa na wategemezi wao.
Akizungumza kwa niaba ya wanafamilia nyengine 9, mmoja ya
ndugu wa marehemu hao, Ame Ramadhani amesema misaada na ushirikiano wanaopatiwa na
taasisi mbali mbali za umma na binafsi inawafariji na kuwapunguzia uchungu wa
kuondokewa na jamaa zao ambao walikuwa wakiwategemea kimaisha.
Ramadhan alieleza hayo baada ya
kupokea misaada mbali mbali jkutoka kwa kampuni ya halotel na kuishukuru kampuni hiyo
kwa msaada huo
ambao alisema umekuja kwa wakati muafaka.
“Tunaishukuru ofisi ya Mkuu wa mkoa
wa Mjini Magharibi kwa kuonesha kujali hali zetu baada ya kuondokewa na
wapendwa wetu kwani toka tumepatwa na msiba huu imekuwa mstari wa mbele
kutafuta misaada na inapopatikana inatukabidhi bila ya kujali wingi au uchache
wake”, alieleza Ramadhan.
Awali akizungumza kwa niaba ya mkuu
wa mkoa wa mjini magharibi mara
baada ya kupokea
misaada hiyo kutoka kampuni
ya Halotel Katibu
Tawala Mkoa wa Mjini Magharibi Hamida Mussa Khamis katika ofisi za mkoa huo Vuga, alisema
serikali ya mkoa inafanya hivyo kwa kuthamini kazi iliyokuwa ikifanywa na
askari hao na inathamini misada hiyo ambayo inatoa faraja kwa familia za askari
hao, serikali na wanajeshi kwa ujumla.
“Tunaomba msichoke kila tutakapowaita
kwani tunajua kidogo mnachopokea hakilingani na maisha ya ndugu na jamaa zenu
ambao wamefariki wakipigania haki na amani kwa jamii. Hivyo sisi tuliobaki
tunaona njia pekee ya kuenzi juhudi zao ni kutafuta kila aina ya msaada kwenu”,
alisema hamida na kuushukuru uongozi wa kampuni ya Halotel kwa msaada huo.
Mkurungezi Msaidizi wa
kampuni hiyo kanda ya Zanzibar
Abdallah Iddi alisema kampuni yake imeamua kutoa msaada huo wa
fedha taslim kwa kila familia ili kuzifariji na kurudisha sehemu ya faida
wanayoipata kutokana na shughuli zao hapa Zanzibar.
Mnamo mwezi Novemba mwaka
uliomalizika askari 15 wa JWTZ walifariki dunia baada ya kushambuliwa wakiwa
sehemu ya jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa liliopo nchini Congo DRC ambapo wanajeshi 10 kati yao walizikwa sehemu mbali mbali za Zanzibar akiwemo askari mwengine
aliefariki mwezi uliopita nchini Uganda alipokuwa anapatiwa
matibabu kutokana na shambuluio hilo.
Katibu Tawala Mkoa wa Mjini Magharibi Hamida Mussa Khamis akizungumza na wanafamilia za maaskari 10 za askari wa JWTZ (hawapo pichani) kabla ya kuwakabidhi msaada wa fedha taslim na fulana uliotolewa na kampuni ya Halotel kwa lengo la kuwafariji.
Mmoja wa wanafamilia za askari 10 wa JWTZ Ame Ramadhan (kushoto) akipokea msaada kota kwa mmoja ya maafisa waandamizi wa kampuni ya halotel kanda ya Zanzibar kwa ajili ya kuwafariji kutokana na msiba wa ndugu na jamaa zao waliofariki dunia nchini DRC Congo.
No comments:
Post a Comment