Na Mwinyimvua Nzukwi
MIRADI 49 ya kiuchumi, maendeleo na ustawi wa jamii
inatarajiwa kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi wakati wa shamra shamra za
maadhimisho ya miaka 54 ya mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar balozi seif ali
iddi ameeleza hayo baada ya kikao cha cha Halmashauri ya Sherehe na Maadhimisho
ya Kitaifa anayoiongoza.
Alisema miongoni mwa miradi hiyo, 33 itazinduliwa
rasmi baada ya kukamilika wakati miradi mingine 16 inatarajiwa kuwekewa Mawe ya
msingi inayojumuisha miradu ya taasisi za umma, miradi ya Jamii sambamba na ya Wawekezaji vitega uchumi.
Katika kikao hicho kilichofanyika katika makumbusho
ya kasri la Mfalme, Balozi Seif na wajumbe wa halmashauri hiyo walifikia
maamuzi ya kuipunguza miradi mitatu iliyoainishwa katika ratiba ya sherehe hizo
baada ya kubaini kuwa haikufikia kiwango kinachokubalika.
Kaimu Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Kanali Said Khamis
Said ambae ni mjumbe wa kikao hicho, alisema kutakuwa na mabadiliko katika gwaride
la mwaka huu kutokana na kilele cha sherehe hizo kuangukia katika siku ya Ijumaa hivyo
gwaride hilo litamalizika mapema ili kutoa fursa kwa wananchi na viongozi
kujiandaa na ibada ya sala ya Ijumaa.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Dk. Idriss Muslim Hijja alisema miradi yote iliyopendekezwa kuingizwa
katika maadhimisho ya Mwaka huu imefuatiliwa na kutolewa taarifa kwa sekriterieti
na kufanyiwa marekebisho kwa kiwango kinachohitajika kuingizwa katika ratiba ya
sherehe.
Katika hatua nyengine waziri wan chi ofisi ya makamo
wa pili wa rais wa Zanzibar Mohammed Aboud Mohammed amewaambia waandishi wa
habari ofisini kwake jana kuwa wastani wa shillingi billion 1.2 zinatarajiwa
kutumika kwa ajili ya maadhimisho ya sherehe za miaka 54 ya mapinduzi matukufu
ya Zanzibar yatakayofikia kilele chake Januari 12, mwakani.
Aboud amesema serikali imepanga kutumia kiasi hicho
cha fedha kulingana na umuhimu wa siku hiyo ambapo kuelekea katika kilele
chake shughuli mbalimbali za kitaifa na kijamii zitafanyika zikiwemo za kuwekewa
mawe ya msini na kuzinduliwa kwa miradi ya maji, majengo ya skuli, Umeme
na Barabara ambapo viongozi wa SMZ na SMT wanatarajiwa kuizindua
kulingana na ratiba zitakazopangwa.
Aidha waziri Aboud alisema katika siku ya kilele serikali itaeleza jinsi ilivyopiga hatua katika kufanikisha huduma muhimu za kijamii na maendeleo kazi ambayo ni mwendelezo wa malengo ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar yaliyofanyika mwaka 1964.
Aidha waziri Aboud alisema katika siku ya kilele serikali itaeleza jinsi ilivyopiga hatua katika kufanikisha huduma muhimu za kijamii na maendeleo kazi ambayo ni mwendelezo wa malengo ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar yaliyofanyika mwaka 1964.
Kilele cha sherehe hizo kinatarajiwa kuadhimishwa 12
Januari Uwanja wa Amaan ambapo viongozi mablimbali wa kitaifa na kimataifa
wanatarajiwa kuhudhuria akiwemo Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein
atakaekuwa mgeni rasmi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi (kulia) akiongoza kikao cha halmashauri ya sherehe za kitaifa katika ukumbi wa Baraza la Mapinduzi uliopo katika makumbusho ya Kasri ya Mfalme, Forodhani mjini Unguja. (Picha kwa hisani ya OMPR)
No comments:
Post a Comment