Na Mwinyimvua Nzukwi
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud ametoa
wiki moja kwa Uongozi wa Baraza la Manispaa ya Mjini, Idara ya Utunzaji na
Uendelezaji, barabara Zanazibar (UUB) na kampuni ya ZECON kuhakikisha
wanaifanyia matengenezo barabara ya kwa Biziredi - Misufini ambayo imechimbwa
kwa ajili ya kupitisha waya wa umeme na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wake
na wakaazi wa maeneo hayo.
RC Ayoub alitoa agizo hilo katika siku ya sita ya ziara zake ndani
ya mkoa huo kuzungumza na wananchi kusikiliza kero changamoto zinazowakabili
ambapo wananchi wanaoishi katika eneo hilo walilalamikia athari zilizoachwa na
ujenzi huo.
Alifahamisha kuwa utaratibu wa kukata barabara hiyo
haukukamilishwa hivyo aliwataka wahusika wote kuhakikisha wanaifanyia marekebisho
barabara haraka na kulitaka baraza la manispaa kufuatilia majukumu yao kwa wakati
pindi wanapotoa ruhusa ili kuhakikisha azma ya serikali ya kuimarisha miundombinu
inafikiwa kama ilivyokusudiwa.
Aidha Mkuu hoyo wa Mkoa alilitaka Baraza la Sanaa, Sensa ya
filamu na Utamaduni kufuta kibali cha kupiga muziki katika ukumbi wa Maisara CCM
Social Hall baada ya wananchi wanaoishi jirani na ukumbi huo kulalamikia sauti
za muziki jambo ambalo linakiuka agizo la Serikali ya Mkoa Mjini Magharibi la
kutopigwa katka siku za katikati ya wiki.
Katika hatua nyengine, Ayoub amelitaka baraza la Manispaa ya Mjini,
Kamisheni ya Utalii na Bodi ya vileo kutotoa kibali na leseni ya biashara kwa
nyumba ya kulala wageni ya Jambo iliyopo Migombani mjini Unguja kutokana na
kusababisha kero mbali mbali kwa wananchi wa maeneo hayo likiwemo la kutumika
kama danguro.
“Kwa hili la jambo guest house, taasisi zinazohusika na kutoa
vibali na lesini ya biashara naagiza visitolewe hadi tutakapoelewana mwacheni
amalizie muda wake lakini kisitolewe kibali kwa ajili yam waka ujao kwani
hatuwezi kumwacha mtu mmoja anakera wengine kwa kisingizio cha mapato”, alisema.
Awali akiwasilisha malalamiko yake kwa niaba ya wananchi
wenzake mkaazi wa shehia ya Migombani ali khamis mwinyi alieleza kuwa nyumba
hiyo ambayo iana baa ndani yake imekuwa kero kwa wakaazi na wageni wa eneo hilo
kiasi cha kusababisha maafa.
“Kinachotusikitisha watu wanaokwenda katika hiyo gesti kwa
ajili ya ufska baadhi yao hutumia misikiti uliopo jirani na hiyo nyumba kwa
kuoga lakini hutupa mipira ya kiume iliyokwishatumika tunategemea kuwa na jamii
gani?”, alihoji mwananchi huyo.
Akitoa ufafanuzi juu ya malalamiko ya wananchi kuhusu usafiri
wa bodaboda Zanzibar, Katibu wa bodi ya usafiri wa barabarani Mohammed Simba alisema
usafiri huo haujaruhusiwa kwa mujibu wa sheria namba 7 ya mwaka 2003 kwa ajili
ya kusafirisha abiria na kuwepo kwake ni kinyume na sheria za nchi.
Hata hivyo alieleza kuwa sheria imetoa ruhusa kwa bodi yake
kumshauri waziri anaehusika na masuala ya usafirishaji juu ya vyombo vinavyowea
kutumika kwa ajili ya usafiri na usafishaji wa abiria hivyo wanaendelea
kufuatilia kuona kama ipo haja ya aina hiyo ya usafiri kuruhusiwa.
Mkuu wa Mkoa wa Majini Mgharibi Unguja Ayoub Mohammed Mahamoud (kushoto) akitoa maelekezo baada ya kupokea malalamiko ya wananchi katika uwanja wa Komba wapya mjini Unguja.
katibu wa biodi na mahakama ya vileo zanzibar (katikati) akijibu hoja na kutoa ufafanuzi kuhusiana na Baa na nyumba ya kulala wageni ya Jambo iliyopo Migombani baada ya wananchi wa shehia hiyo kuilalamikia. kulia ni mwananchi alietoa malalamiko hayo ali khamis mwinyi na wa kwanza kushoto waliosimama ni mkurugenzi wa manispaa ya Mjini Abou Serenge. (PICHA KWA HISANI YA OFISI YA MKUU WA MKOA).
No comments:
Post a Comment