Na Mwinyimvua Nzukwi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi na kuwabadilisha nafasi baadhi ya viongozi wa Taasisi mbali mbali za Serikali ya Zanzibar akiwemo aliyekua Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mwanajuma Majid Abdallah.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi na kuwabadilisha nafasi baadhi ya viongozi wa Taasisi mbali mbali za Serikali ya Zanzibar akiwemo aliyekua Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mwanajuma Majid Abdallah.
Mwanajuma alieshika hatamu za uongozi wa Mkoa huo kwa muda
mrefu, ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Kazi, Uwezeshaji,
Wazee, Wanawake, Vijana na Watoto anayeshughulikia masuala ya Wazee, Vijana,
Wanawake na Watoto.
Kufuatia mabadiliko hayo, Dk. Shein amemteua Hemed Suleiman
Abdullah kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini- Pemba, Hassan Khatib Hassan kuwa Mkuu wa
Mkoa wa Kusini, Unguja kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Muslih Hija
alieteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa wizara ya nchi ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar.
Aidha katika mabadiliko hayo Rais pia amemteua aliekuwa Katibu
Tawala wa Wilaya ya Magharibi B Hamida Mussa Khamis kuwa Katibu Tawala wa Mkoa
wa Mjini Magharibi na Mohamed Abdulla Ahmed kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya
Magharibi.
Wengine walioteuliwa ni Daima Mohamed Mkalimoto alieteuliwa kuwa
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti katika Ofisi ya Rais,
Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuchukua nafasi ya Abdulla
Issa Mgongo anaekua Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti
katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za
SMZ.
Aliekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar
(BTMZ) Sharifa Khamis Salim ameteuliwa kuwa Kamishna wa Idara ya Michezo katika
Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo na Mohamed Issa Mugheir
ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ya Zanzibar
uteuzi ambao umeanza Disemba 5, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment