Na Mwinyimvua Nzukwi
Makamo wa Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA - Unguja) Mzee
Zam Ali ameteuliwa kuwa mjumbe katika kamati itakayosimamia Mashindano ya
Chalenji yaliyoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati
(CECAFA) yanayotarajiwa kuanza Disemba 3
hadi 17 mwaka huu nchini Kenya.
Taarifa iliyotolewa na CECAFA imeeleza kuwa Zam ambaye
aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa ZFA kwa muda mrefu imeeleza kuwa imefikia uamuzi
huo kutokana na uzoefu alionao katika Mashindano mbali mbali yakiwemo
mashindano hayo.
Wajumbe wengine waliochaguliwa kuunda kamati hiyo ni
Mutasim Gafar kutoka nchini Sudan, Abdigaan Arab Said kutoka Somalia, Jacob
Odundo kutoka Kenya, Ashinafi Ejigu wa Ethiopia, Aimable Habimana wa Burundi,
Rogers Byamukama wa Uganda, Ajong Domasio Ajong wa Sudan ya Kusini na Ahmed
Mgoyi kutoka Tanzania Bara.
Wajumb wengine na nchi wanazotoka katika mabano ni Sunday
Kayuni (Tanzania Bara), Mossi Yussuf (Burundi), Celestine Ntangugira (Rwanda),
Yigzaw Ambaw (Ethiopia), Bernard Mfubusa (Burundi), Maxim Itur (Kenya), Rogers
Mulindwa (Uganda), Bonny Mugabe (Rwanda), Gishinga Njoroge (Kenya), Amir Hassan
(Somalia) na Nicholas Musonye (Kenya).
Mashindano hayo yanatarajiwa kushirikisha timu 10 za Tanzania bara,
Zanzibar, Kenya, Rwanda na wageni waalikwa Libya zilizopo katika kundi 'A' wakati kundi 'B' linaundwa na timu za Sudani ya Kusini, Ethiopia, Burundi, Uganda na wageni
waalikwa Zimbabwe.
No comments:
Post a Comment