NA
MWINYIMVUA NZUKWI, ZANZIBAR
Mkurugenzi wa mawasiliano na matukio ya kijamii wa kampuni ya vinywaji baridi ya Coca cola Tanzania Haji Mzee Ally ameeleza kuwa kampuni yake itaendelea kudhamini mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari tanzaniz UMISETA kutokan na kuridhishwa na matokeo yake.
Haji alieleza hayo mara baada ya kuzinduliwa kwa mashindano hayo kwa skuli za Zanzibar na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud katika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Alisema ili kusaidia upatikanaji wa viwango bora na wachezaji katika michezo mbali mbali, kampuni hiyo itaendelea kudhamini michezo sio tu kwa kufanya hivyo kunaakisi malengo ya kampuni yake, bali pia malengo ya taifa ya kuongeza ajira kupitia sekta ya michezo ambao imeajiri watu wengi katika siku za karibuni.
“Tulipoanza kudhamini mashindano haya miaka miwili iliyopita tulilenga kuongeza hamasana, ushindani na kuleta mabadiliko katika sekta ya michezo kitu ambacho tunaamini tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa baada ya tahmini yetu kunesha kupatikana kwa matokeo chanya katika baadhi ya michezo ukiwemo mpira wa miguu”, alisema Haji.
Alieleza kuwa mbali ya kudhamini mashindano hayo yanayojumuisha michezo mingi pia kampuni yake inadhamini mashindano ya vijana katika mchezo wa soka jambao ambalo alidai limeleta mafanikio makubwa kwa mchezaji mmoja mmoja, klabu na taifa kwa ujumla.
mapema akifungua mashindano hayo, mkuu wa mkoa Mhmoud aliyataka makampuni na
mashirika binafsi kama Coca cola kuunga mkono juhudi za serikali ya Zanzibar katika
kukuza vipaji vya wanamichezo kwa kudhamini michezo mbali mbali ili kuleta
maendeleo ya jamii.
Mahmoud alisema serikali ya Zanzibar kupitia Wizara ya elimu na mafunzo ya amali Zanzibar imeanzisha mpango wa
kukuza michezo katika skuli 55 unatambulika kama ‘Sports 55’ unaolenga kuibua
na kuviendeleza vipaji vya wanafunzi wanamichezo ili kutoa matokeo bora kama
ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.
Alisema katika
utekelezaji wa mpango huo serikali imejidhatiti kuzalisha walimu, waamuzi,
upatikanaji wa vifaa vya michezo na kujenga viwanja katika kila wilaya
kitakachoweza kutumiwa kwa ajili ya michezo zaidi ya mmoja.
“Toka ameingia
madarakani Rais wa Zanzibar amekuwa akihimiza uwepo wa vuguvugu la michezo ili
kuirudishia nchi yetu (Zanzibar) hadhi yake katika medani ya michezo jambo
ambalo linapaswa kuungwa mkono na kila mmoja wetu katika nafasi aliyopo”,
alisema Mahmoud.
Aidha Mkuu huyo
wa mkoa aliipongeza kampuni ya Cocacola kwa kuamua kudhamini mashindano ya UMMISETA
kwa mwaka wa 3 mfululizo na kuwaasa walimu na wanafunzi kuvitunza vifaa
vilivyotolewa ili viweze kutumika kwa muda mrefu.
“Mnapofanya hivi
sio tu mnasaidia juhudi za serikali katika kuimarisha michezo nchini bali pia
mnajikaribisha kwa jamii kwani hiki mnachokuifanya ni sehemu ya kurudisha faida
mnayoipata kwao kitu ambacho kinapaswa kuzingatiwa na taasisi nyengine”,
alieleza Mahmoud.
Awali akitoa
taarifa katika tukio hilo, Mkurugenzi wa kamisheni ya michezo na utamaduni wa
wizara ya elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Hassan Tawakal Khayrallah alisema
skuli 20 zitapatiwa jezi, viatu na mipira kwa ajili ya maandalizi ya mashindano
ya kanda kabla ili kupata timu zitakazoshirikia mashindano ya UMISETA taifa
yatakayofanyika baadae mwaka huu mjini Mwanza.
Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohamed Mahmoud (katikati) akishiriki mazoezi na wanafunzi wa darasa la elimu ya mazoezi la skuli ya Mwanakwerekwe ‘C’ kabla ya kuzindua mashindano ya UMISETA kanda ya Zanzibar. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa kamisheni ya michezo na utamaduni Hassan Khairallah Tawakal na Mkurugenzi wa mawasiliano na matukio ya kijamii wa Coca cola Haji Mzee Ally. Wa kwanza kutokea kulia ni mwalimu wa darasa hilo Othman Ali.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud akisalimiana na waamuzi wa mchezo wa uzinduzi wa mashindano ya UMISETA kanda ya Zanzibar uliozikutanisha timu za skuli ya Lumumba Sekondari na Regeza Mwendo sekondari. Kutoka kulia ni Suleiman Adhuhuri Ibrahim (14) aliyekuwa mwamuzi msaidizi namba 1, Hamiyar Muhsin Ali (14) aliyekuwa mwamuzi wa akiba, Aboubakar Khatib Omar (13) mwamuzi wa kati na Rashid Ramadhan Ahmada (15) aliekuwa mwamuzi wa msaidizi namba 2.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud (kulia)
akimkabidhi mmoja ya walimu wa skuli 20 za Zanzibar vifaa vya michezo kwa ajili
ya mashindano ya UMISETA kanda ya Zanzibar. Anaeshuhudia ni Mkurugenzi wa
kamisheni ya elimu na utamaduni Zanzibar Hassan Khairallah Tawakal.
Mkurugenzi wa mawasilano na matukio ya kijamii wa kampuni ya coca cola Tanzania Hjai Mzee Ally (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud zawadi ya mpira uliotumika katika uzinduzi wa mashindano ya UMISETA kanda ya Zanzibar uliofanyika April 20, 2018 katika uwanja wa amaan Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud (kulia) akipiga dana
dana kwa ampira aliokabidhiwa kama zawadi na Mkurugenzi wa mawasiliano na
matukio ya kijamii wa kampuni ya Coca cola Haji Mzee Ally (kulia). Kushoto ni
Mkurugenzi wa Kamisheni ya michezo na utamaduni wa wizara ya elimu na mafunzo
ya amali Zanzibar Hssan Khairallah Tawakal.
No comments:
Post a Comment