Wednesday, April 25, 2018

NMB YAOMBWA KUZISAIDIA TAAISISI ZA UMMA, BINAFSI

NA MWINYIMVUA NZUKWI, ZANZIBAR
Taasisi za fedha nchini zimetakiwa kuendelea kuzisaidia taasisi za umma na binafsi kuuweka mifumo mizuri ya matumizi ya fedha ili kusaidia maendeleo ya taasisi hizo na taifa kwa ujumla.

Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud alitoa wito huo wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya siku mbili yaliyoshirikisha wakuu wa taasisi za serikali, mashirika ya umma, taasisi za kiraia na vyuo vya elimu ya juu yaliyoandaliwa na benki ya NMB Tanzania.

Amesema iwapo taasisi hizo zitajengewa uwezo zitaimarisha mifumo yao ya mapato na matumizi jambo litakalosaidia kukuza mapato yao na kudhibiti matumizi kulingana na mageuzi ya kiuchumi kupitia mifumo mipya ya kifedha ya kitaifa na kimataifa.

Amesema serikali ya Zanzibar kupitia Mkakati wa Kupunguza Umaskini Zanzibar (MKUZA I, II,III) imefanya mabadiliko kadhaa katika sektambali mbali ikiwemo ya sekta ya fedha yaliyolenga kukuza mapato ya serikali, mashirika ya umma na taasisi zisizo za kiraia hivyo taasisi hizo zinapaswa kuhakikisha zinatumia huduma za kibenki zinazotolewa na benki hiyo ili kujiendeleza.

“Nchi haiwezi kuendelea kama hakutokuwepo na mifumo mizuri ya kifedha nah ii ndio maana serikali ikaamua kufanya marekebisho katika sheria zake ili kuruhusu sekta za fedha zuiweze kutoa huduma bora zitakazosaidia makundi mbali yaweze kunufaika nazo”, amesema Mahmoud.

Nao washiriki wa mafunzo hayo walisema kuwa yamewasiadia kujua huduma mbali mbali za kifedha zinazotolewa na benki hiyo sambamba na kuwajengea uwezo ambao watautumia katika kutafuta vyanzo vipya vya mapato na kudhibiti matumizi yao kwa manufaa ya wanachama wa taasisi hizo na jamii kwa ujumla.

Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa bodi ya chama cha wanasheria wanawake Zanzibar ZAFELA Fatma Gharib ameeleza kuwa mafunzo hayo yamewashajihisha kutumia huduma mbali mbali za kifedha kama vile kupata ushauri na mikopo inayotolewa kwa taasisi zisizozalisha faida jambo ambalo litasaidia kuziimarisha taasisi hizo kuwa na maendeleo endelevu.

“Taasisi zetu (za kiraia) kimsingi huwa zinategemea ruzuku au misaada na kujua kuwa wajibu wetu katika matumizi ya benki ni kutunziwa fedha jambao ambalo kupitia semina hii nimeiona fursa pana zaidi ya hiyo ambayo taasisi zetu inaweza kuitumia kupitia benki hii”, aamesema Fatma.  

Akitoa maelezo kuhusu mafunzo hayo mkuu wa biashara za kitaasisi kutoka makao makuu ya benhi ya NMB William Makoresho amesema mafunzo hayo yalilenga kuonesha shughuli zinazofanywa na benki yake kwa baadhi ya wateja wake ili waweze kuzitumia kwa lengo la kuimarisha utendaji wa taaisisi hizo.

“Watu wengi wanafikiria benki yetu inafanya kazi ya kutunza fedha au kutoa mikopo kwa wateja wetu pekee lakini kupitia semina hii tumeweza kuwaelezea washiriki ukubwa huduma na faida zinazoweza kupatikana na sisi kuweza kujua mahitaji ya wateja wetu hivyo ningependa kuwaalika waendelee kutumia huduma za benki na kifedha zinazotolewa na benki yetu”, amesema Makoresho.

Nae Meneja wa benki hiyo tawi la Zanzibar Abdallah Duchi amesema mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa benki hiyo kuyafikia makundi mbali ya kijamii ili kuwaelezea umuhimu wa kutumia huduma za kifedha katika kukuza uchumi wa taasisi na kwamba katika mafunzo benki hiyo iliwafikia Wakurugenzi wa taasisi na mashiriika ya serikali, Wakurugenzi wa taasisi za kiraia na Wakuu wa taasisi za elimu ya juu ili kuwajengea uwezo juu ya namna bora ya kuongeza mapato na tija ya taasisi zao.

 Meneja wa tawi la NMB Zanzibar Abdallah Duchi (wa pili kutoka kushoto) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud (wa pili kulia) kuhusu semina ya watendaji wakuu wa taasisi za serikali, mashirika ya umma na asasi za kiraia kabla ya Mkuu huyo kufunga rasmi mafunzo hayo.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud (kushoto) akihutubia washiriki wa semina ya wakuu wa taasisi za serikali, mashirika ya umma na asasi za kiraia yaliyoandliwa na benki ya NMB. Kulia ni Mkuu wa huduma za Biashara za Taasisi wa benki ya NMB William Makoshero.


Baadhi ya washiriki wa semina ya wakuu wa taasisi za serikali, mashirika ya umma, taasisi zisizo za kiserikali na vyuo vya elimu ya juu (waliosimama) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud (wa pili kulia waliokaa) mara baada ya kufunga semina hiyo.

Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud (wa tatu kulia) akijadiliana jambo na Meneja wa NMB Zanzibar Abdallah Duchi (wa pili) na mkuu wa biashara za kitaasisi William Makoshero.

Meneja wa NMB Zanzibar Abdallah Duchi (kulia) akiagana na Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud mara baada ya kufunga semina ya wakuu wa taasisi za serikali, mashirika ya umma, taasisi zisizo za kiserikali na vyuo vya elimu ya juu iliyofanyika katika hoteli ya Verde, Mtoni Zanzibar.

Friday, April 20, 2018

COCA COLA YAAHIDI KUENDELEA KUPIGA TAFU MICHEZO, RC AYOUB ATAKA WADAU WENGINE WASAIDIE KUINUA VIPAJI


NA MWINYIMVUA NZUKWI, ZANZIBAR
Mkurugenzi wa mawasiliano na matukio ya kijamii wa kampuni ya vinywaji baridi ya Coca cola Tanzania Haji Mzee Ally ameeleza kuwa kampuni yake itaendelea kudhamini mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari tanzaniz UMISETA kutokan na kuridhishwa na matokeo yake.

Haji alieleza hayo mara baada ya kuzinduliwa kwa mashindano hayo kwa skuli za Zanzibar na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud katika uwanja wa Amaan Zanzibar.

Alisema ili kusaidia upatikanaji wa viwango bora na wachezaji katika michezo mbali mbali, kampuni hiyo itaendelea kudhamini michezo sio tu kwa kufanya hivyo kunaakisi malengo ya kampuni yake, bali pia malengo ya taifa ya kuongeza ajira kupitia sekta ya michezo ambao imeajiri watu wengi katika siku za karibuni.

“Tulipoanza kudhamini mashindano haya miaka miwili iliyopita tulilenga kuongeza hamasana, ushindani na kuleta mabadiliko katika sekta ya michezo kitu ambacho tunaamini tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa baada ya tahmini yetu kunesha kupatikana kwa matokeo chanya katika baadhi ya michezo ukiwemo mpira wa miguu”, alisema Haji.

Alieleza kuwa mbali ya kudhamini mashindano hayo yanayojumuisha michezo mingi pia kampuni yake inadhamini mashindano ya vijana katika mchezo wa soka jambao ambalo alidai limeleta mafanikio makubwa kwa mchezaji mmoja mmoja, klabu na taifa kwa ujumla.

mapema akifungua mashindano hayo, mkuu wa mkoa Mhmoud aliyataka makampuni na mashirika binafsi kama Coca cola kuunga mkono juhudi za serikali ya Zanzibar katika kukuza vipaji vya wanamichezo kwa kudhamini michezo mbali mbali ili kuleta maendeleo ya jamii.

Mahmoud alisema serikali ya Zanzibar kupitia Wizara ya elimu na mafunzo ya amali Zanzibar imeanzisha mpango wa kukuza michezo katika skuli 55 unatambulika kama ‘Sports 55’ unaolenga kuibua na kuviendeleza vipaji vya wanafunzi wanamichezo ili kutoa matokeo bora kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.

Alisema katika utekelezaji wa mpango huo serikali imejidhatiti kuzalisha walimu, waamuzi, upatikanaji wa vifaa vya michezo na  kujenga viwanja katika kila wilaya kitakachoweza kutumiwa kwa ajili ya michezo zaidi ya mmoja.

“Toka ameingia madarakani Rais wa Zanzibar amekuwa akihimiza uwepo wa vuguvugu la michezo ili kuirudishia nchi yetu (Zanzibar) hadhi yake katika medani ya michezo jambo ambalo linapaswa kuungwa mkono na kila mmoja wetu katika nafasi aliyopo”, alisema Mahmoud.

Aidha Mkuu huyo wa mkoa aliipongeza kampuni ya Cocacola kwa kuamua kudhamini mashindano ya UMMISETA kwa mwaka wa 3 mfululizo na kuwaasa walimu na wanafunzi kuvitunza vifaa vilivyotolewa ili viweze kutumika kwa muda mrefu.

“Mnapofanya hivi sio tu mnasaidia juhudi za serikali katika kuimarisha michezo nchini bali pia mnajikaribisha kwa jamii kwani hiki mnachokuifanya ni sehemu ya kurudisha faida mnayoipata kwao kitu ambacho kinapaswa kuzingatiwa na taasisi nyengine”, alieleza Mahmoud.

Awali akitoa taarifa katika tukio hilo, Mkurugenzi wa kamisheni ya michezo na utamaduni wa wizara ya elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Hassan Tawakal Khayrallah alisema skuli 20 zitapatiwa jezi, viatu na mipira kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya kanda kabla ili kupata timu zitakazoshirikia mashindano ya UMISETA taifa yatakayofanyika baadae mwaka huu mjini Mwanza. 













Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Mohamed Mahmoud (katikati) akishiriki mazoezi na wanafunzi wa darasa la elimu ya mazoezi la skuli ya Mwanakwerekwe ‘C’ kabla ya kuzindua mashindano ya UMISETA kanda ya Zanzibar. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa kamisheni ya michezo na utamaduni Hassan Khairallah Tawakal na Mkurugenzi wa mawasiliano na matukio ya kijamii wa Coca cola Haji Mzee Ally. Wa kwanza kutokea kulia ni mwalimu wa darasa hilo Othman Ali.

 
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud akipiga mpira kuashiria ufunguzi wa mashindano ya UMISETA kanda ya Zanzibar. Uzinduzi huo ulifanyika jana katika uwanja wa amaan Zanzibar. Wa pili kutoka kulia ni mwamuzi mstaafu wa kimataifa (FIFA) Ramadhan Ibada Kibo anaesimamia mafungo wa mafunzo ya waamuzi watoto.


Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud akisalimiana na waamuzi wa mchezo wa uzinduzi wa mashindano ya UMISETA kanda ya Zanzibar uliozikutanisha timu za skuli ya Lumumba Sekondari na Regeza Mwendo sekondari. Kutoka kulia ni Suleiman Adhuhuri Ibrahim (14) aliyekuwa mwamuzi msaidizi namba 1, Hamiyar Muhsin Ali (14) aliyekuwa mwamuzi wa akiba, Aboubakar Khatib Omar (13) mwamuzi wa kati na Rashid Ramadhan Ahmada (15) aliekuwa mwamuzi wa msaidizi namba 2.
 

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud (kulia) akimkabidhi mmoja ya walimu wa skuli 20 za Zanzibar vifaa vya michezo kwa ajili ya mashindano ya UMISETA kanda ya Zanzibar. Anaeshuhudia ni Mkurugenzi wa kamisheni ya elimu na utamaduni Zanzibar Hassan Khairallah Tawakal.


Mkurugenzi wa mawasilano na matukio ya kijamii wa kampuni ya coca cola Tanzania Hjai Mzee Ally (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud zawadi ya mpira uliotumika katika uzinduzi wa mashindano ya UMISETA kanda ya Zanzibar uliofanyika April 20, 2018 katika uwanja wa amaan Zanzibar.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud (kulia) akipiga dana dana kwa ampira aliokabidhiwa kama zawadi na Mkurugenzi wa mawasiliano na matukio ya kijamii wa kampuni ya Coca cola Haji Mzee Ally (kulia). Kushoto ni Mkurugenzi wa Kamisheni ya michezo na utamaduni wa wizara ya elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Hssan Khairallah Tawakal.



Thursday, April 19, 2018

BAMMATA LATAKIWA KUWAENDELEZA WANAMICHEZO WAKE


NA MWINYIMVUA NZUKWI
Wajumbe wa Kamati Tendaji ya Baraza la Michezo la Majeshi ya Tanzania – BAMMATA wametakiwa kutumia weledi katika uongozi wa michezo ili kuhakikisha wanasimamia shughuli za maendeleo ya michezo katika vyombo vya ulinzi na usalama bila ya kuathiri sheria na kanuni za michezo husika.

Akifungua kikao cha Kamati hiyo katika ukumbi wa mikutano wa idara ya uhamiaji Zanzibar mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud alisema kufanya hivyo kutathibitisha ubora wa vyombo hivyo katika medani ya michezo na ulinzi wa nchi.

KAMATI YA UONGOZI YA TASAF UNGUJA, WATENDAJI WAOMBA WASHIRIKIANE


NA MWINYIMVUA NZUKWI
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini TASAF III Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud amewataka wajumbe wa Kamati hiyo kuzidisha mashirikiano na watendaji wa mpango huo ili utekelezaji wake uoneshe matokeo yanayopimika.

Akizungumza katika Mkutano wa kutathmini utekelezaji wa mpango huo katika kipindi cha mwaka 2017, uliofanyika katika ofisi za TASAF Mazizini Unguja, alisema kufanya hivyo kutasaidia kupunguza changamoto zilizobainika ikiwemo ya kutopatikana kwa matokeo yaliyotarajiwa katika baadhi ya miradi inayotekelezwa.

Monday, April 16, 2018

RC AAGIZA MICHEZO KUHIMIZA AMANI


NA MWINYIMVUA NZUKWI
Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud amewataka washiriki wa mbio za baskeli za Afrika Mashariki kutangaza vivutio vya utalii viliopo na amani ya nchi za afrika mashariki  ili kukuza uchumi wan chi hizo unaotegemea pato la utalii.

Akihutubia wananchi na washiriki wa mbio hizo katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, RC Ayoub amesema mbio hizo zikitumika kusambaza na kueneza ujumbe wa amani zitasaidia kuwashawishi na kuwakumbusha wananchi juu ya umuhimu wa kulinda amani iliyopo pamoja na uhifadhi wa mazingira kwa lengo la kuimarisha utalii wa ndani wa Zanzibar na Tanzania bara.

Amewataka washiriki hao wanaotoka katika nchi mbali mbali za ukanda wa Afrika Mashariki, Kati na Kusini kutumia muda mchache watakaokuwepo Zanzibar kupitia vivutio vya utalii vilivyopo na kwenda kuvitangaza katika nchi zao sambamba na kuelezea hali ya amani iliyopo nchini.

Aidha aliishukuru wizara ya Habari, Utamaduni na Mambo ya Kale kwa kuamua kushirikiana na taasisi ya Afrika Mashariki Festival kwa kuamua kuanzisha mbio hizo ndani ya mkoa wa Mjini Magharibi mbio ambazo zinatarajiwa kufanyika pia katika mkoa wa Dar es salam ambazo amesema zitasaidia kukuza uwekezaji katika sekta mbali mbali ikiwemo ya utalii.

Mapema akitoa taarifa za mbio hizo katibu mtendaji wa kamisheni ya utalii Zanzibar Dkt. Vuai Idi Lila amezitaja nchi zilizotoa washiriki wa mbio hizo kuwa Tanzania bara, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, afrika kusini na wenyeji Zanzibar.

Amesema mbio hizo ni sehemu ya mikakati ya kamisheni yake ya kuimarisha utalii nchini katika majira yote kama moja ya azma ya serikali ya Zanzibar pamoja na kukuza uhusiano na wadau wengine wa utalii nchini.

Jumla ya washiriki 72 wakiwemo wanawake wawili kutoka nchini Kenya walishiriki mbio hizo za umbali wa kilomita 60 zilizoanzia katika uwanja wa Amaan kupitia Welezo, Mwera, Dunga, Jendele, Unguja Ukuu, Bungi, Tunguu na kurudia  njia ya Mwera hadi uwanja wa Amaan.
Washiriki wa mbio za baskeli za afrika mashariki wakijiandaa kuanza mbio hizo.

Mkuu wa mkoa wa mjini magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud akipeperusha bendera ya jumuiya ya afrika mashariki kuashiria kuanza kwa mbio za baskeli za Afrika Mashariki


Mmoja kati ya wanawake wawili walioshiriki mbio hizo kutoka nchini Kenya.


Sunday, April 15, 2018

BALOZI SEIF AONYA UKATAJI WA MITI, AIPONGEZA ZAFRED KUCHIMBA VISIMA


NA OTHMAN KHAMIS, OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameinasihi jamii kuepuka kukata miti ovyo na badala yake irejee katika utamaduni ya kuotesha miti katika maeneo wanayoishi ili ardhi iendelee kubakia katika maumbile yake ya kawadia.
Alisema hivi sasa kiwango cha maji katika ardhi kinaendelea kupungua kutokana na tabia ya wanaadamu kuchafua mazingira ikiwemo ukataji ovyo wa misitu jambo ambalo ni hatari kwa maisha ya viumbe.
Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Mwakilishi wa jimbo la Mahonda alitoa nasaha hizo wakati wa sherehe za uzinduzi wa visima viwili vya maji safi na salama vilivyochimbwa katika kituo cha afya jimbo la Donge na skuli ya msingi na sekondari za Mahonda jimbo la Mahonda.

'ZANZIBAR OLD STARS' YATAKA WENYE MAMLAKA YA SOKA LA ZANZIBAR WAWATUMIE


Na Salum Vuai, MAELEZO
TIMU ya soka ya wachezaji wa zamani Zanzibar Old Stars, imemuomba Mkuu wa Mkoa wa Mjini  Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud, kusaidia kuwaelimisha wadau  na mamlaka za michezo juu ya umuhimu wa kutunza kumbukumbu zinazohusiana na mchezo huo nchini.

Akizungumza wakati uongozi wa timu hiyo ulipokwenda kumshukuru Mkuu huyo na kumkabidhi kikombe cha ushindi wa mechi ya ‘Karume Day’, Katibu Mkuu wa kikosi hicho Salum Hamduni, alisema inasikitisha kuona wanasoka walioiletea sifa Zanzibar hawathaminiwi hata kwa kutakiwa ushauri.

Alisema tafauti na nchi nyengine, Zanzibar haina utaratibu wa kutunza historia za wanamichezo wake wa zamani ambao waliiwakilisha kimataifa na kuifanya itambuliwe na kuheshimiwa ndani na nje ya nchi.

Saturday, April 14, 2018

WANACHAMA CCM WAHIMIZWA KULINDA MISINGI YA VYAMA VYA ASP NA TANU


Na Is-Haka Omar, Zanzibar.
WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameshauriwa kuendeleza harakati za kulinda, kutetea na kusimamia misingi ya taasisi hiyo ili kuenzi kwa vitendo juhudi za waasisi wa ASP na TANU.
Hayo ameyasema Katibu Mwenezi CCM Wilaya ya Dimani Hassan Suleiman  Jaku,  katika ziara ya Makatibu uenezi wa CCM ngazi za matawi hadi Wilaya ya Dimani walipotembelea  maeneo ya historia ya kumbukumbu ya aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar marehemu Abeid Aman Karume,  Kisiwandu Unguja. 
Makatibu wenezi wakipata maelezo ndani ya chumba alichouawa muasisi wa mapinduzi ya Zanzibar Sheikh Abeid Aman Karume.
Amesema nguvu za Chama Cha Mapinduzi zinatokana na wanachama wazalendo wanaolinda na kuthamini urithi wa Chama hicho toka enzi za vyama vya ASP na TANU.

WAZEE ZANZIBAR WAMPONGEZA DK. SHEIN KWA KUENDELEZA PENCHENI JAMII, WAMUOMBA KUPUNGUZA UMRI WA WANUFAIKA WANAWAKE



Na Mwinyimvua Nzukwi
Jumuiya ya Wazee Zanzibar (JUWAZA) imeiomba serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kupunguza umri wa wazee wanawake wanaopokea pencheni jamii kutoka  miaka  75 hadi 55 ili kuliwezesha kundi hilo kunufaika na pencheni hiyo.

Wakizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kutimiza miaka miwili toka kuanza kutolewa kwa pencheni hiyo, wazee hao walimshukuru Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein kwa kuanzisha pensheni hiyo waliyosema imesaidia kuimarisha hali zao na kuondokana na utegemezi.