NA MWINYIMVUA NZUKWI
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Rikizi Pembe
Juma amewataka wananchi wa mkoa wa Mjini Magharibi kushirikiana na
ofisi ya Mkuu wa mkoa huo katika
kuimarisha usafi na upendezeshaji wa mji ili uendelee kuwa kivutio kwa wageni
na wenyeji.
Akizungumza katika hafla ya uzinduizi wa bustani ya
kihistoria iliyopo mbele ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo, waziri Riziki ameeleza kuwa uhifadhi
wa eneo hilo utasaidia kuweka mazingira ya mji na kuwa kivutio kikubwa
kwa wageni wanaoingia nchini.
Amesema wageni wengi wanaoingia nchini huvutiwa na
historia ya mji mongwe wa Zanzibar ambao ni miongoni mwa miji ya urithi wa
kimataifa hivyo uhifadhi wa eneo hilo kunaongeza uhai wa histopria ya zqanzibar
na eneo hilo.
“Eneo hili pamoja na kuwa na ofisi bado linaweza
kutumika na wananchi kujipumzisha hivyo ni wajibu wa wafanyakazi
na wananchi wanaofika katika eneo hili kuhakikisha wanashirikiana
katika kuitunza bustani hii”, alieleza Waziri Riziki.
Aidha amewaomba wafanyabiashara
na taasisi nyengine kuunga mkono kwa kuchangia juhudi zinazochukuliwa na
serikali ya mkoa wa mjini magharibi katika ukuzaji wa maendeleo ya jamii na
kuipongeza benki ya Diamon Trust kwa kufadhili ujenzi na uimarishaji wa bustani
hiyo.
“Sote tunaziona juhudi za mkuu wa mkoa na viongozi
wenzake wanavyopigania maendeleo ya jamii hasa katika masuala ya elimu, hivyo
ninawaomba watu wenye uwezo na mapenzi mema kuendelea kumuunga mkono ili kuweka
mazingira mazuri ya kujifuzia kama njia moja wapo ya kuimarisha ubora wa elimu
ya watoto wetu na maendeleo ya taifa”, alisema.
Akitoa taarifa katyika hafla hiyo iliyofanyika
mbele ya ofisi yake, Mkuu wa mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud alisema
ujenzi wa bustani hiyo umekuja ili kutimiza ahadi iliyowekwa na serikali ya
mkoa kwa rais wa Zanzibar ya kuendelea na upendezashi wa mji kupitia manispaa za wilaya zote
tau za mkoa huo.
Alisema wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar Dk. Ali
Mohamed Shein mwaka uliopita, mkoa huo pamoja na mambo mengine uliahidi
kuendelea kuimarisha usafi wa mji na kuuweka katika hali ya kupendeza hivyo
alizitaka manispaa hizo kuhakikisha zinasimamia sheria na kanuni dhidi ya watu watakaoharibu mazingira ya maeneo mbalimbali ya
mkoa huo.
“Tulipotoa ahadi ile mbele ya Rais (Dk. Ali Mohamed
Shein) tulikuwa tunaaamini kuwa tutaweza kufikia lengo la kuziweka vizuri
bustani zetu lakini pia kuimarisha usafi wa maeneo yetu jambo ambalo
tunashukuru wadau wa maendeleo kama DTB (Diamond Trust Bank) wameziona juhudi
zetu na kuamua kutuunga mkono”, alisema Ayoub na kuishukuru benki hiyo kwa
uamuzi wake huo.
Nae Mkuu wa kitengo cha
masoko wa benki ya DTB Sylester Bahati akizungumza katika hafla
hiyo alisema benki yake itaendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar katika sekta maeneo mbali mbali ikiwemo sekta elimu
ili kuhakikisha wanachangia maendeleo ya serkta hiyo na jamii kwa
ujumla.
Ujenzi wa bustani hiyo ulioanza katikati ya mwaka
uliopita na kukamilika hivi karibuni, mbali ya kuwema vigae katika eneo la kuegesha
magari pia umehusiaha upandaji wa maua na miti ya asili ya Zanzibar na kuweka
vibaraza vya kupumzikia ulifadhiliwea na Benki DTB Tawi la Zanzibar kwa gharama
ya shilingi milioni 45.
No comments:
Post a Comment