Monday, November 26, 2012

AFUTA HATI YA UMILIKI WA ARDHI

BALOZI SEIF ASITISHA UMILIKI WA ARDHI
  • ATAKA MASLAHI YA WANYONGE YAZINGATIWE
  • ATAKA WANANCHI, MAMLAKA KUHESHIMU SHERIA
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefuta hati ya umiliki wa eneo la shamba la serikali alilomilikishwa  Abeid Said Shankar liliopo katika kijiji cha Selemu wilaya ya magharibi Unguja.

Hatua hiyo imefikiwa kufuatia mgongano unaoendelea kujitokeza kati yake na wanakijiji wa eneo hilo ambao unaashiria uvunjifu wa amani baina ya mmiliki huyo na wanakijiji hao.
Aidha hatua hiyo pia inauzuia uongozi wa kituo cha kujiendeleza kielimu katika shehia hiyo kufanya shuguli yoyote ya ujenzi kwa kile kilichogundulika kuwa umiliki wa eneo hilo hauko kihalali katika vyombo vinavyosimamia masuala ya Ardhi.
Zuio hilo limetolewa hivi karibuni na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofanya ziara fupi katika eneo hilo baada ya malalamiko ya muda mrefu ya wananchi wanaotumia maeneo hayo hao dhidi ya watu wanaodaiwa kumilikishwa mashamba hayo ambayo yalikuwa yakitumiwa na wizara ya kilimo.
Naibu katibu mkuu wa Wizara Kilimo na Maliasili Juma Ali Juma alimthibitishia Makamu wa Pili wa Rais kwamba mmoja ya watu wanaodai kumiliki eneo hilo Kassim Hassan hakuwa na nyaraka halali za eneo hilo ambalo ni lilikuwa ni milki ya Wizara ya Kilimo walilopewa baada ya mapinduzi ya ya Zanzibar ya 1964.
Juma alisema kutokana na maombi na umuhimu wa ardhi kwa mahitaji ya jamii, serikali imeiagiza wizara hiyo kupima eneo hilo ili baadae ligaiwe kwa wananchi kwa lengo la kuendeleza mahitaji ya kilimo na ujenzi kazi ambayo alisema kuwa imeshakamika.
Malalamiko ya wanachi yalikwenda sambamba na ule mzozo unaofukuta kati ya wakulima waliokuwa wakiendeleza shughuli za Kilimo katika shamba la Bwana Abeid Said wakidai kwamba mmiliki huyo alikuwa akionyesha dalili mbali mbali za kuhatarisha maisha ya mifugo yao pamoja na vipando vyao.
Akitoa ufafanuzi wa kadhia hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliiagiza wizara ya kilimo kumtafutia shamba jengine Bwana Abei Said Shankar ili kuepuka shari.
“Nakuagizeni Wizara ya Kilimo mhakikishe kuwa mnampatia eneo la kujenga nyumba mwananchi huyu masikini wa Mungu, mnampimia eneo la ujenzi Bwana Kassim kwa ajili ya kituo chao waweze kumiliki kihalali pamoja na kumpatia shamba jengine bwana Abeid" aliagiza balozi Iddi na kuongeza kuwa hatua hii itaondoa mvutano bila ya migongano miongoni mwa jamii.
“Kama mtu anashindwa kuishi na jamii inayomzunguka katika maeneo ya umiliki wa serikali mtu huyo inafaa aondoshwe na mamlaka zinazosimamia umiliki huo wa Serikali ili kuepuka shari”. Alisisitiza Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar.
Aidha Balozi Seif aliiasa jamii kuheshimu sheria na taratibu zilizowekwa ili kuepuka mizozo isiyokuwa na lazima na kutahadharisha kwamba ardhi itaendelea kuwa mali ya serikali na haitasita kuitumia kwa maslahi ya umma.
Eneo hilo la ekari sita lililopo katika kijiji cha Selemu, wilaya ya Magharibi, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja kilichojaaliwa utajiri wa ardhi yenye  rutba lililomilikishwa kwa wizara ya kilimo na mali asili Zanzibar tokea mwaka 1964.

CHANZO: OMPR

Tuesday, November 6, 2012

MAHAFALI YA PILI FUONI

 "TUSHIRIKIANE KUSAIDIA SEKTA YA ELIMU KWA MAENDELEO YA TAIFA" - BAUCHA 
 
Wadau wa elimu nchini wametakiwa kutoa mashirikiano kwa walimu ili kuinua kiwango cha ufaulu wa wanafunzi na ubora wa elimu inayotolewa katika skuli za serikali na binafsi nchini.
Akizungumza katika mahafali ya pili ya wanafunzi wa skuli ya Fuoni Sekondari waliomaliza kidatu cha nne Mkurugenzi wa biashara wa kampuni ya Zantel Moh’d Khamis Baucha alisema mashirikiano kati ya pande hizo ndio njia pekee itakayoongeza kiwango cha kufaulu na kuleta ufanisi kwa jamii nzima.
Alisema kuwa katika zama za sayansi na teknolojia ni lazima kuwepo na njia mbadala zitakaziowezesha wanafunzi kunufaika na elimu wanayoipata wakiwa skuli kama njia mojawapo ya kujikomboa na umasikini na kujitegemea pindi wanapomaliza masomo.
“Zama zimebadilika sana, ipo haja kwa wanafunzi, walimu, wazazi na wadau wengine kushirikiana na kuhakikisha tunazingatia katika upatikanaji wa elimu bora na sio bora elimu tu”, alisema.
Aidha aliwaasa wahitimu hao kuhakikisha wanayatumia vyema mafunzo waliyoyapata wakati wanasubiri matokeo na kuwa raia wema huku wakiwasaidia wanafunzi wanaoendelea situu kujua kusoma bali pia kufahamu wanachosomeshwa.
“Wakati mkiondoka skuli ni vyema mkayatumia masomo mliyoyapata na kuwasaidia wenzenu waliobaki kujua kusoma, kufahamu wanachosomeshwa, na kuhesabu kama njia ya kujijengea uwezo wenu na wao katika kufikiri na kupambanuua mambo,….. mkifikia hatua hiyo mtakuwa mmeelimika kikamilifu”, aliongeza Meneja huyo.
Aidha aliahdi kuwa kampuni yake italishughulikia tatizo la ukosefu wa vifaa vya maabara na kompyuta linaloikabili skuli hiyo na kuwataka wadau wengine kujitokeza kusaidiaskuli hiyo hususan uchakavu wa majengo ili kupata mazingira mazuri ya kujifunzia jambo ambalo amedai lina mchango mkubwa katika upatikanaji wa elimu bora.
“Nimesikia kilio chenu, kwa kuanzia nimekuja na ‘modem’ za ‘internet’ kwa ajili ya mtandao na nitakaa na wenzangu katika kampuni kuangalia ni namna gani tunaweza kusaidia hasa masuala ya vifaa vya maabara na kompyuta ili kuendana na wakati uliopo”, alisema Meneja Baucha.
Akisoma risala ya walimu na wanafunzi wa skuli hiyo, Mwalimu Sudi Mchenga alizitaja changamoto za uhaba wa walimu hasa katika masomo ya sayansi, uchakavu wa majengo, uhaba wa samani, vifaa vya maabara na kompyuta kuwa ni miongoni mwa mambo yanayokwaza malengo yao ya kufaulisha, wanafunzi wengi zaidi kila mwaka.
“Pamoja na kupiga hatua za mafanikio mwaka hadi mwaka, bado uchakavu wa majengo, samani na nyenzo nyengine za kujifunzia na kufundishia zimekuwa ni matatizo yanayotukwaza kufikia malengo yetu, hivyo tunawaomba wadau wote kutusaidia ili tutimize wajibu wetu kikamilifu”, alisema Maalim Mchenga.
Mapema akimkaribisha mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa idara ya elimu sekondari Zanzibar, Maalim Ali Hamdani aliwataka wanafunzi wanaofaulu kuendelea na elimu ya juu nchini kufanya maombi mapema katika bodi ya mikopo ya elimu ya juu ili kuepusha malalamiko ya kunyimwa mikopo.
“Idadi ya wanafunzi wanaohitaji mikopo imekuwa ikiongezeka kila mwaka hivyo basi wale watakaobahatika kuendelea na masomo hasa ya elimu ya juu ni vyema wakafanya maombi mapema kabla bajeti haijapitishwa ili kuweza kutoa mikopo kwa wanafunzi wengi zaidi”, alisema afisa huyo akijibu ombi la kupatiwa mikopo kwa walimu wanaokwenda kusoma.
Aidha aliwataka walimu wanaopata nafasi ya kwenda kusoma kurudi maskulini mwao ili kupunguza uhaba wa walimu ambao amedai unachangiwa na baadhi yao kutorudi katika vituo vyao wanapomaliza masomo na wengine kubadilisha kada kwa kisingizio cha maslahi duni jambo ambalo alisema linachangia kupunguza idadi ya walimu.
Skuli ya Fuoni ni miongoni mwa skuli kongwe zilizopo Zanzibar iliyoanzishwa mwaka 1952 ikitoa elimu ya awali ,msingi ha kati kabla ya kubadilishwa kuwa ya sekondari, katika mahafali hayo wanafunzi 129 wanaume 58 na wanawake 71 walikabidhiwa vyeti vya kumalizia masomo idadi ambayo ni ziada ya wanafunzi 16 ya wanafunzi 113 waliomaliza mwaka jana ambapo kati yao wanafunzi 11, wanawake 7 na wanaume 4 walifaulu na kuendelea na kidato cha tano katika skuli mbali mbali.

SORAGA AMWAGIWA TINDIKALI


KATIBU WA MUFTI ZANZIBAR AMWAGIWA TINDIKALI


Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga amemwagiwa tindikakali na watu wasiojulikana asubuhin ya leo wakati akiwa mazoezini huko maeneo ya viwanja vya Mwanakwerekwe, nje kidogo ya manispaa ya mji wa Zanzibar.

Habari zilizopatikana asubuhi hii ni kwamba mara baada ya kutokea kwa tukio hilo, Sheikh alikimbizwa katika hospitali ya Mnazi mmoja ambako alipatiwa huduma ya kwanza kabla ya kusafirishwa kwa ndege ya serikali katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi. Hadi sasa hakuna fununu au watu waliokamatwa au kuhusishwa na tukio hilo.

Pichani, Sheikh Fadhil Soraga akitolewa katika Chumba cha Huduma ya Mwanzo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kabla ya kusafirishwa kwenda katika hospitali ya muhimbili jijini Dar es salam kwa matibabu zaidi.

Monday, October 29, 2012

ZIARA YA MAKAMO WA 2 WA RAIS SMZ

 
                                                                                                                                                                                                  NAKAGUA:
Mnamo oktoba 28, 2012 Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alifanya ziara ya siku moja kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeleo iliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi na kufadhiliwa na serikali au washirika wa maendeleo.
Ziara hiyo ilihusisha vijiji vya Bweleo, Fumba na Bwefum viliopo wilaya ya Magharibi, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja. Haya ni baadhi ya matukio katika ziara hiyo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia majengo ya skuli ya Bwefum iliyoko Wilaya ya Magharibi, Mkoa wa  Mjini Magharibi ambayo Mapaa yake yako katika hali ya uchakavu akiwa na Mwalimu Mkuu wa Skuli hiyo Kesi Mwinyi Shomari pamoja na baadhi ya wanafunzi wa darasa la kwanza wa skuli hiyo.
 
 Mwalimu mkuu wa skuli ya Bwefum, Kesi Mwinyi Shomari (wa kwanza kushoto aliyevaa kofia) akimuongoza Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi kukagua majengo na eneo la skuli hiyo siku kiongozi huyo alipotembelea vijiji vya Bweleo na Fumba kukagua miradi ya maendeleo na chanagamotozinazowakabili wananchi wa vijiji hivyo.
 
 
Mmiliki wa eneo lenye  Magofu ya Bwefum, Bwana Chandra (wa kwanza kulia) akitoa maelezo kwaa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi kufuatia mgogoro wa muda mrefu kati yake na Wananchi wa Kijiji Hicho. Balozi Seif alizitaka pande hizo kuwa na subra wakati Serikali inafanya utafiti utakaopelekea kupatikana kwa maamuzi sahihi ya kusuluhisha mgogoro huo.
 
Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi wa Uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu wa kijiji cha  Bweleo, Hassan Gharib (wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi juu ya changamoto wanazoipambana nazo katika kutimiza azma yao. Wa kwanza kulia alievaa miwani ni mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Zanzibar (BTMZ) Sharifa Khamis.
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifurahia bidhaa zilizotengenezwa na Kikundi cha Ushirika cha Ukweli ni Njia Safi cha Kijiji cha Bweleo. Kikundi hicho kinazalisha bidhaa mbali mbali za matumizi ya urembo na kawaida kwa kutumia mwani na mazao mengine ya baharini hali iliyomshawishi makamo huyo wa Rais kununua baadhi ya bidhaa hizo.




Wednesday, October 17, 2012

HAKI YA KUJUA

SIKU YA HAKI YA KUJUA DUNIANI
  • JUKWAAA LA KUTATHMINI UWAJIBIKAJI KWA WOTE
  • TAARIFA SAHIHI NA ZA WAKATI CHACHU YA MAENDELEO YA JAMII

Na: Mwinyimvua Nzukwi, Zanzibar

Septemba 28, kila mwaka inatambuliwa kimataifa  kuwa ni siku ya haki ya kujua duniani.

Siku hiyo ilianzishwa mwaka 2002 huko Sofia, Bulgaria kufuatia mkutano wa vyombo na sekta za habari uliojadili namna bora ya kutumikia umma kwa lengo kuongeza uwajibikaji na uelewa wa mtu mmoja mmoja juu ya haki zao kwa serekali pia wajibu wa serekali na vyombo vyake kwa wananchi wake.

Tabaani siku hii ina umuhimu wa pekee kwa pande zote mbili, serikali kwa upande mmoja na wananchi kwa upande mwingine na bila shaka ndipo haja ya kusimikwa na kusimamiwa kwa sheria zinazolazimisha watu kutoa na wengine kupata habari inapoanzia.

Kama zilivyo nchi nyingi duniani Tanzania iliadhimisha siku hii kwa mikutano ya wadau mbali mbali wa habari kwa lengo la kujuzana na kukukmbushana juu ya dhima ya kila mmoja katika jamii ya kufanya juhudi ya kujua hususan mambo ya msingi katika jamii yake.

Mambo hayo yanaweza kuwa ni haki na wajibu wa serikali na vyombo vyake kwa umma, wajibu wa raia kwa serikali na hata wenyewe kwa wenyewe, namna ya uendeshaji wa dola, mipaka ya utawala kati ya ngazi moja na nyengine na kadhalika.

Katika mkutano ulioandaliwa na Baraza la Habari Tanzania ofisi ya Zanzibar, uliofanyika katika hoteli ya Mazson, haki ya kujua imetajwa kuwa ni miongoni mwa haki za msingi za binadamu inayoanzia toka mtu anapokuwa mdogo na kuendelea nayo kadri anavyokuwa.

Akitoa mada juu ya umuhimu wa haki ya kujua Katibu Mtendaji wa tume ya utangazaji ya Zanzibar, Chande Omar Omar aliitaja haki hii kuwa hukua hatua kwa hatua toka katika hali ya mtoto kujitambua maumbile yake, watu anaohusiana nao na kufikia kiwango cha kujua ni kwa nini mambo yako kama yalivyo na si vyenginevyo.

"Tunapofikia hapo ndipo haja ya kujua inakuwa imefikia kiwango cha kuleta mabadiliko katika jamii na hii inatokana na uwezo wa kudadisi na kutafuta ukweli juu ya mambo mbali mbali", alisema Chande.

Aliongeza kuwa hali hii haitokei kwa bahati mbaya bali huwa ni kipaji anachozaliwa nacho mtu na namna alivyokuzwa na familia yake au alivyopata fursa zenye kukuza upeo wa kufikiri na kupembanua mambo.

"Uwezo wa kuhoji unatokana na jinsi makuzi aliyoyapata mtoto ......... iwapo mtoto alikuwa anapatiwa fursa ya kuhoji na kupata majibu yanayostahiki, bila shaka atakuwa na uthubutu wa kutaka kujua kila jambo linalotokea nchini hata kama taarifa zake zitakuwa zimefichwa", aliongeza Chande na kuwataka vijana kutokuwa na hofu ya kuhoji, kudadisi na kutafuta ukweli kwa lengo la kujua kwani kufanya hivyo ni kuitekeleza haki yao kikatiba.

"Msiogope. Section 18 (kifungu cha 18) ya katiba ya Zanzibar ipo wazi juu ya haki ya kutafuta na kupata habari, tafuteni na hamtozuiwa ......... yule atakaewazuia bila shaka atakuwa hajui na mtakapomjulisha mtakuwa mmetekeza wajibu wenu", aliongeza Chande.

Akichangia mada hiyo mtangazaji wa kituo cha redio cha Chuchu FM, Mulhat Yussuf Said alisema tabia ya viongozi wa taasisi za serikali ya kuficha au kubagua kutoa taarifa kwa vyombo vya binafsi inawakosesha wananchi walio wengi haki ya kujua mambo kwa wakati kutokana na vyombo hivyo kuwa na wasikilizaji wengi na kutoa matangazo yao kwa muda mwingi na kwa wakati.

"Baadhi ya viongozi wa taasisi za umma wana tabia ya kuficha habari au kubagua vyombo vya kuzipa habari hasa sisi tunaofanya kazi katika vyombo binafsi.... hii sio sawa kwani kuna kundi kubwa hasa vijana ambao husikiliza vyombo hivi" alisema bi Mulhat.

Akitolea mfano wa madhara ya kutojua, afisa kutoka tume ya ukimwi Zanzibar (ZAC) Dk. Sihaba Saadati alisema kukosekana taarifa sahihi na kwa wakati kulichangia kwa kiasi kikubwa kuenea kwa maradhi ya ukimwi katika baadhi ya maeneo nchini jambo ambalo lingeweza kudhibitiwa kama taarifa zingeliwafikia watu kwa muda muafaka.

"Mwanzoni taarifa kuhusu ukimwi zilikuwa hazipatikani kirahisi lakini baada ya kuanza kutolewa tumeona jinsi watu wanavyochukua tahadhari juu ya kuambukizwa au hata tiba yake kwa wale waliambukizwa jambo ambalo limesaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti kasi ya maambukizi mapya", alisema afisa huyo.

Nae mwandishi mwandamizi Salim Said Salim alieleza kuwa ni makosa kwa viongozi wa vyombo na taasisi za serikali kuficha na kukalia taarifa kwa umma na kufanya hivyo ni kwenda kinyume na taratibu na sheriazanchi.

"Zipo taarifa haziwezi kutolewa na kuhojiwa hadharani lakini kwa zile taarifa za kawaida ni makosa kuzikalia au kuweka urasimu katika upatikanaji wake kwani hizi ni taarifa za umma na watu wanahaki ya kujua", alisema Said.

Alitolea mfano wa upatikanaji wa taarifa za tenda zinazotolewa na serikali au taasisi zake katika kutoa huduma mbali mbali kuwa haziwekiwi wazi jambo linalopelekea kuwepo kwa upendeleo na ubadhirifu wa mali za umma huku wanachi wa kawaida wakipata tabu.

"Utakuta kiongozi wa taasisi fulani anakalia taarifa kama vile ni mali yake binafsi, hata wafanyakazi wake hawajui kitu na anakuwa mkali pale anapohojiwa. Huu si uendeshaji mwema wa nchi kwani kila mmoja anawajibu wa kuchangia ujenzi wa taifa sasa kama hawajui namna mambo yalivyo watachangiaje?" , alihoji nguli huyo katika fani ya uandishi wa habari.

Mbali ya ubinafsi na ukiukwaji wa taratibu za utawala wa nchi unaofanywa na viongozi wa taasisi mbali mbali za serikali, wachangiaji wengi katika mkutano huo walilitaka Baraza la Habari Tanzania (MCT) kuchepuza mchakato wa upatikanaji wa sheria ya haki ya kupata habari ambayo katika rasimu yake sehemu ya tatu inaelezea haki ya habari na majukumu ya mamlaka za umma katika kustawisha mwenendo wa utoaji na upatikanaji wa habari.

Bila shaka hapo ndipo nchi itakuwa inatekeleza kwa vitendo azimio la umoja wa mataifa la kuanzishwa kwa siku hii ya haki ya kujua kwa kila mmoja katika jamii kutekeleza wajibu wake ipasavyo kwa kupata, kutoa na kusambaza habari kwa wote na kwa wakati.

Baadhi ya wadau wa habari waliohudhuria maadhimisho ya siku ya haki ya kujua yaliyofanyika 28/9/2012 katika ukumbi wa Hoteli ya Mazson mjini Zanzibar wakifuatilia kwa makini mada ya umuhimu wa kujua iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa tume ya utangazaji zanzibar Chade Omar (hayupo pichani). Kutoka kushoto mstari wa mbele ni Mwalim, Juma Seif kutoka idara ya elimu mbadala, Mulhat Said Mtangazaji Chuchu FM redio na Masudi Saanani mwandishi Mwananchi Communication.

Meneja wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) ofisi ya Zanzibar, Suleiman Seif Omar akitoa maelezo ya utambulisho kwa wadau wa habari (hawapo pichani) waliohudhuria maadhimisho ya siku ya haki ya kujua yaliyofanyika 28/9/2012 katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Mazson, Shangani mjini Zanzibar, wengine kutoka kushoto ni Katibu mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Chande Omar Omar, Makamo mwenyekit mstaafu wa MCT Maryam Hamdan na afisa wa fedha na usuluhishi wa MCT Alan Nlawa

Tuesday, October 16, 2012

NIPENI MUDA KUTATUA MGOGORO HUU - BALOZI SEIF


  • MGOGORO WA ARDHI KATI YA JWTZ, WANANCHI NGOMA BADO MBICHI
  • TUME YA TAKRIMA YASHINDWA KUTOA RIPOTI
Na: Mwinyimvua Nzukwi, Zanzibar.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeeleza kuwa inakusudia kutoa uamuzi wa moja kwa moja katika kutafuta suluhu juu ya mgogoro wa ardhi uliopo kati ya Wananchi wa Vijiji vya Fuoni, Maungani , Kombeni na Diiman kwa upande mmoja na Kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kambi ya Kisaka saka wilaya ya magharibi, unguja.

Kauli hiyo imetolewa na makamo wa pili wa rais wa Zanzibar, Balozi Seif Aili Iddi alipokuwa akizungumza na wananchi wa Maeneo hayo katika Kituo cha Afya cha Fuoni Kibondeni baada ya Tume aliyoiunda mwezi Julai mwaka huu kushindwa kuwasilishwa ripoti yake tokea mwishoni mwa mwezi Agosti.

Balozi Iddi aliwataka Wananchi hao kuendelea kuwa na subra wakati Serikali inalitafakari suala hilo kwa ajili ya kulipatia ufumbuzi wa kudumu utakaoleta afueni kwa pande zote mbili.

Aidha aliekleza kusikitishwa kwake kwa kutotekelezwa kwa maagizo aliyoyatowa katika Kikao cha pamoja kati ya pande mbili za mzozo huo mnamo  Julai 7 mwaka huu ambapo mbali na kuunda kamati ya kuchunguza na kupendekeza hatua za kutatua mgogoro huo pia aliuagiza Uongozi wa Kambi ya Kisakasaka kulirejesha Bambo waliloliondoa mahali walipokubaliana na Wananchi katika mazungumzo ya awali.
“ Hakukuwa na haja ya kutoa maamuzi ya haraka kuhusiana na Mgogoro huo, ndio maana nikaunda Tume hiyo lakini cha kusikitisha hadi sasa sijaletewa ripoti hiyo kama nilivyoagiza kuletewa mwishoni mwa Mwezi wa Agosti mwaka huu.” Aliswema Balozi Seif.

Alieleza kuwa Serikali isingependa kuona Jeshi lililoundwa kwa ajili ya kutumikia Jamii linaendelea kuwa na mifarakano na Wananchi katika utekelezaji wa majukumu yake.
Makamu huyo wa Rais wa Zanzibar ambaye ndiye mtendaji na msimamizi mkuu wa shughului za serikali ya Zanzibar aliwaahidi Wananachi hao kwamba mambo yote waliyokubaliana na Uongozi wa Jeshi yanatekelezwa kikamilifu huku ufumbuzi wa kudumu ukitafutwa.
“Nipeni muda, hivi sasa nimetingwa na shughuli za Baraza la Wawakilishi na nadhani mnaelewa kuwa mimi ndie msimamizi mkuu wa kazi za serikali shughuli za Serikali …….. nikimaliza tu jibu la suala hili nitajuka kulitoa hapa hapa”. Alifafanua Balozi Seif.
Mapema Mwenyekiti wa Kamati ya Wananchi hao Khamis Vuai Makame, aliiomba Serikali kuyachukulia hatua za haraka mambo waliyokubaliana na uongozi wa jeshi hilo ili kutatua mgogoro huo na kuepusha madhara yanayoweza kutokea.
Khamis alisema bado wataendelea kulalamikia kutokuwepo kwa uhalali wa ramani ya kambi hiyo wakati wananchi hao ndio wenye hati ya umiliki wa ardhi hiyo kwa mujibu wa sheria na taratibu za mamlaka inayohusika na ardhi hapa nchini walizopatiwa miaka kadhaa iliyopita.
Mwenyekiti huyo alimuelezea Balozi Seif kuwa jeshi hilo limeingia katika mgogoro huo kwa utashi wa baadhi ya watu maslahi yao na si maslahi ya jeshi au jamii inayolizunguka kambi hiyo.
Khamis alisema wanaamini kuwa utatuzi wa mgogoro huo utapatikana kwa kutumia vikao halali na kumpongeza Balozi Seif kwa hatua anazoendelea kuchukuwa katika kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo toka ulipozuka.
“Hapa hapana tatizo kubwa kama tutatumia vikao na kulizungumza kwani mwisho wa yote naamini suluhu itapatikana ”, alisema mwenyekiti huyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliunda tume ya kuufuatilia Mgogoro huo wa ardhi kati ya JWTZ  kambi ya Kisakasaka na wananchi wanayoizunguuka kambi hiyo Julai mwaka huu chini ya uenyekiti wa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi, tume ambayo imeshindwa kuwasilisha ripoti yake katika muda uliopangwa kama iliyoagizwa. .
Mgogoro huo umezuka baada ya wananchi wa vijiji hivyo kulalamikia ramani mpya ya JWTZ inayoonesha maeneo hayo kuwa ni sehemu ya jeshi hilo kambi ya Kisakasaka huku wananchi hao wakiwa na hati halali za umiliki jambo linalodaiwa ni utashi wa baadhi ya watu kwa maslahi yao na si ya taasisi hiyo, madai ambayo yanapingwa na viongozi wa jeshi.
 
551.jpg569.jpgBaadhi ya wananchi wa vijiji vya Fuoni, Maungani , Kombeni na Dimani Wilaya ya Magharibi, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja wakimsikiliza Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar (hayupo pichani) katika mkutano ulioandaliwa kwa lengo la kutafuta suluhu ya mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa vijiji hivyo na JWTZ kambi ya Kisakasaka.

Balozi Seif akisisitiza jambo kwa wananchi wa vijiji vya Fuoni, Maungani, Kombeni na Dimani Wilaya ya Magharibi, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja katika mkutano wa kutafuta suluhu ya mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa vijiji hivyo na JWTZ kambi ya Kisakasaka. (Picha na OMKPR)

Tuesday, September 11, 2012

MIRADI YA JAMII


Na: Mwinyimvua Nzukwi, Zanzibar

MIRADI YA MAENDELEO YA JAMII

Miradi mingi ya kijamii inayoanzishwa kupitia programu mbali mbali za kitaifa zina lengo la kuinua hali za maisha ya wananchi, hivyo basi ipo haja kwa wananchi hao kupewa fursa za kujadili, kupanga na hatimae kuanzisha miradi hiyo kwa lengo la kuifanya kuwa endelevu na tija kwao na jamii kwa ujumla.

Hali ni tofauti katika sehemu nyingi nchini Tanzania na ukweli ni kwamba miradi mingi imeibuliwa na ‘Waheshimiwa’ kwa lengo la kuwasaidia wananchi bali unapotizamza kwa undani utagundua  kuwa miradi hiyo ni mitaji yao kisiasa na kupelekea miradi hiyo kufa na mengine kusuasua bila ya kufikia malengo, kama ulivyo mradi huu wa ufugaji wa mbuzi wa maziwa katika shehia ya Dole, Wilaya ya Magharibi, Mkoa wa Mjini Magharibi .

Pichani ni bi Fatma Bakari akiwa katika kutekeleza majukumu yake ya kutafuta malisho kwa ajili ya mbuzi hao na picha ndogo akionesha mwenendo wa mapato na matumizi yanayotokana na mradi huo ambapo ilibainika kuwa hakuna uwiano kati ya gharama za uendeshaji za mradi huo na tija inayopatikana kiasi cha kuwakatisha tamaa baadhi ya wanachama na kuamua kujitoa.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiiHeYgd4xZTa46__84qbPZVaBo0cmGOiU4IV34aSgDu-mYfsv420KhJiHj5u89X1t6m7yI-CAk7sey-uY0IM-luJq00FWSxIW8TvefBZm757xRVebyTAPZOEso8_Ac04wAKkLAryQiTAr9/s1600/MAN+ZNZ+EXH.jpg

Monday, September 10, 2012

msaada kwa viongozi wa baadae




https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEggo3iNFPwqM5UMnFVeVrBJp8_QKpZh8Af2ujqEoJu9w7UtILjnjKpvD4ltQXOQMdCASnPZmtliOpuSWsIqPpANjbj0bvMddlYx-Dl7EDwibvRXyMwlSP3tRrJ2SKMw6JLP69Rp0Dc8SyI/s1600/DSCN1635.JPG
UJENZI WA TAIFA LOLOTE HUANZA NA MSINGI IMARA AMBAO NI ELIMU BORA KWA WATU WAKE.

ELIMU BORA BILA SHAKA HAITOPATIKANA KWA KUWA NA WALIMU WAZURI PEKEE BALI PIA MAZINGIRA MAZURI YA KUSOMEA YAKIWEMO MADARASA, MADAWATI NA VIFAA VYA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA.

HAWA WAMEANZA NA TUWAUNGE MKONO BASI ILI TUPATE VIONGOZI WENYE KUJUA WAJIBU WAO KWA NCHI YAO NA WATU WAKE.

KWA PAMOJA TUNAWEZA KUZITAMBUA NA KUZITUMIA TUNU ZA TAIFA BILA YA KUGOMANA WALA KUGOMBANIA, TUANZE BASI.

ELIMU BORA KWA WATANZANIA BORA.

Friday, September 7, 2012


TMF ANNOUNCES 2012 FELLOWS

TO ALL MEDIA PRACTITIONER
August 03, 2012 
After a competitive vetting process, the Tanzania Media Fund (TMF) has finally selected ten journalists to participate in the Fellowship Programme slated to start in early September, 2012. The ten scribes were picked following oral and written interviews from a group of 27 short-listed candidates from Tanzania mainland and Zanzibar. A total of 70 journalists had applied.

The selected journalists with their media outlets in brackets are as follows; Kulwa Magwa (Uhuru Publications Limited), Fred Okoth (New Habari (2006) Ltd), Frank Leonard (Tanzania Standard Newspapers Ltd) and Joas Kaijage (Mwananchi Communications).

Others are Gordon Kalulunga (Freelance journalist), Maryam Mkumbaru (Uhuru Publications Limited), David Azaria (Tanzania Standard Newspapers Ltd), Irene Mark (Free Media Limited), Stella Mwaikusa (Jambo Concepts Tanzania Limited) and Swaum Mustapher (Tanzania Standard Newspapers Ltd).

This year’s fellowship focuses on three specialized areas – the extractive industry (oil and gas), maternal health and business and economic reporting. Last year’s major was on agriculture and environment.

“I’m really delighted for having been selected as a fellow and will do my best to ensure I deliver accordingly and in the process enrich my skills through the mentorship and experience that I will get,” says David Azaria, a correspondent with Habari Leo/Daily News in Geita region.

To Irene Mark of Tanzania Daima newspaper, the fellowship is bound to change her approach in looking at news and tackling issues of public interest. “I stand to gain a lot from this programme, considering that it is tailored in a manner that encourages one to specialize on a subject of interest. I want to be an authority on maternal health issues,” says Irene.

Giving an overview of the entire process to getting the final ten fellows, the Director of TMF, Ernest Sungura said this year’s applicants were many and the process very competitive.

The fellowship programme was introduced two years ago with a view to bridging the existing rural-urban gap in media coverage.  It encourages journalists to write in-depth articles on specialized areas for a period of six months. TMF gives the fellows a modest stipend, covers transport costs and equipment during the fellowship.

AZIMIO LA DAR ES SALAM

WAANDISHI WATAKA AZIMIO LIWAFIKE WADAU WOTE


Na Mwinyimvua Nzukwi, Zanzibar
Waandishi wa habari nchini walitaka baraza la habari Tanzania kuendelea kulielimisha wadau mbali mbali wa sekta ya habari juu ya azimio la Dar es salaam kuhusu uhuru wa uhariri na uwajibikaji wa wadau wanaochangia uanzishwaji na uendeshaji wa vyombo vya habari.

Wakichangia mada washiriki wa mafunzo ya siku tatu kuhusu maadili ya vyombo vya habari wamesema wamiliki, wafanyabiashara na wanasiasa wanachangia wamekuwa wakandamizaji na wavunjaji wakubwa wa maadili ya uandishi na waandishi wa habari jambo linalochochea kuporomoka hadhi ya taaluma ya habari.

“Pamoja na uzuri wa mafunzo haya kwetu lakini ni vyema baraza likawafanyia na wamiliki wa vyombo tunavyofanyia kazi labda inaweza kupunguza kasi ya ukiukwaji ya maadili yqa fani yetu”, alisema Suzan Kunambi.

Kunambi ambaye pia ni katibu mtendaji wa Zanzibar Press Club alisema suala la maadili ndio msingi wa taaluma na waandishi wanajitahidi kufungamana nalo ila wamiliki na wadau wengine huwa ndio tatizo linalowafanya waandishi kutokuwa na hiyari katika kutii ammri za mabosi wao.

“Utakuta wakati jambo unalijua kuwa ni kinyume na utaratibu, unamwambia mkubwa wako kuwa hivi sivyo lakini anakwambia fanya ninavyotaka, na ukiangalia una njaa ya kazi basi unalazimika kutii japo kwa shingo upande”, aliongeza katibu huyo.

Naye zaituni makwali mwandishi wa kituo cha redio cha chuchu fm alisema kuwasilishwa kwa asimio hilo kwa wadau wote kutasaidia kuongeza uelewa na uwajibikaji wa sekta hiyo kwa maslahi ya jamii na taifa kwa ujumla.

Alisema hatua hiyo itasaidia kupunguza wamesikitishwa na vitendo vya rushwa na upendeleo vinavyoendelea kushamiri katika vyombo vya habari kiasi cha kuwa chanzo cha migogoro miongoni mwa waandishi.

“Utamkuta mkubwa Fulani katika chombo ana urafiki na mtu mwengine sasa anakitumia chombo chake kumpendelea rafiki yake au taasisi yake bila ya kutoa fursa ya mtu mwengine kujitetea, sasa mambo kama haya yanahitaji kuchukuliwa hatua za haraka ili kuzuia mfarakano katika jamii”, alisema.

Akithibitisha kuwepo kwa rushwa katijka vyombo vya habari wmandishi wa star tv abdalla pandu alisema imeshaanza kuota mizizi na hatua za dharura zinahitajika ili kuepusha madhara yanayoelekea kuikumba fani ya habari nchini.

“Waandishi tunapokea rushwa wakati mwengine kwa kujua au bila kujuana wengine wanaomba kabisa na kuchagua kazi za kwenda “ alisema mwandishi huyo na kuongeza kuwa hali hiyo sit u inapunguza heshima ya mwandishi na taaluma yake bali pia inaondoa wajibu wa mwandishi wa habari kwa jamii.

“Mwandishi ni kiyoo cha jamii na anatakiwa kuwa mfano bora kwao sasa inapotokea waandishi kunafanya kazi za ‘mishiko’ je zile za ‘makabwela’ wasio na pesa zitafanywa na nani?”, alihoji Pandu.

Mapema akiwasilisha muhtasari wa mada ya azimio la Dar es Salam juu ya uhuru uhariri na uwajibikaji, mwezeshaji Joyce Bazira alisema azimio hilo linatokana na mabadiliko yanayoikumba sekta ya habari yaliyoibua vitisho vingi katika ipatikanaji wa haki za msingi za binaadamu ikiwemo haki ya kupata habari na kujieleza.
  
Alisema kwa kutambua umuhimu wa vyombo vya habari na mabadiliko yanayoikuma sekta hiyo na wajibu wake kwa jamii ndipo azimio hilo likatolewa ili kuzingatia haja na mahitaji ya makundi yote ya kijamii.
katika kupiga vita suala hilo.

Akitoa mada kuhusiana na azimio hilo mkufuzi wa warsha hiyo maalim Juma Ali Simba alisema hali ya waandishi kuonesha uwajibikaji katika utendaji wa kazi zao ni jambo la lazima kwani bila ya maadili sekta hiyo haitaweza kufikia lengo la kuwa muhimili wa nne wa taifa.

Mafunzo hayo ya siku tatu yaliwashirikisha waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali vya Zanzibar  ikiwa ni hatua za Baraza la Habari Tanzania (MCT) katika kuwasilisha rasimu ya azimio hilo la Dar es saalam lililofikiwa mwaka uliopita.