Friday, September 7, 2012

AZIMIO LA DAR ES SALAM

WAANDISHI WATAKA AZIMIO LIWAFIKE WADAU WOTE


Na Mwinyimvua Nzukwi, Zanzibar
Waandishi wa habari nchini walitaka baraza la habari Tanzania kuendelea kulielimisha wadau mbali mbali wa sekta ya habari juu ya azimio la Dar es salaam kuhusu uhuru wa uhariri na uwajibikaji wa wadau wanaochangia uanzishwaji na uendeshaji wa vyombo vya habari.

Wakichangia mada washiriki wa mafunzo ya siku tatu kuhusu maadili ya vyombo vya habari wamesema wamiliki, wafanyabiashara na wanasiasa wanachangia wamekuwa wakandamizaji na wavunjaji wakubwa wa maadili ya uandishi na waandishi wa habari jambo linalochochea kuporomoka hadhi ya taaluma ya habari.

“Pamoja na uzuri wa mafunzo haya kwetu lakini ni vyema baraza likawafanyia na wamiliki wa vyombo tunavyofanyia kazi labda inaweza kupunguza kasi ya ukiukwaji ya maadili yqa fani yetu”, alisema Suzan Kunambi.

Kunambi ambaye pia ni katibu mtendaji wa Zanzibar Press Club alisema suala la maadili ndio msingi wa taaluma na waandishi wanajitahidi kufungamana nalo ila wamiliki na wadau wengine huwa ndio tatizo linalowafanya waandishi kutokuwa na hiyari katika kutii ammri za mabosi wao.

“Utakuta wakati jambo unalijua kuwa ni kinyume na utaratibu, unamwambia mkubwa wako kuwa hivi sivyo lakini anakwambia fanya ninavyotaka, na ukiangalia una njaa ya kazi basi unalazimika kutii japo kwa shingo upande”, aliongeza katibu huyo.

Naye zaituni makwali mwandishi wa kituo cha redio cha chuchu fm alisema kuwasilishwa kwa asimio hilo kwa wadau wote kutasaidia kuongeza uelewa na uwajibikaji wa sekta hiyo kwa maslahi ya jamii na taifa kwa ujumla.

Alisema hatua hiyo itasaidia kupunguza wamesikitishwa na vitendo vya rushwa na upendeleo vinavyoendelea kushamiri katika vyombo vya habari kiasi cha kuwa chanzo cha migogoro miongoni mwa waandishi.

“Utamkuta mkubwa Fulani katika chombo ana urafiki na mtu mwengine sasa anakitumia chombo chake kumpendelea rafiki yake au taasisi yake bila ya kutoa fursa ya mtu mwengine kujitetea, sasa mambo kama haya yanahitaji kuchukuliwa hatua za haraka ili kuzuia mfarakano katika jamii”, alisema.

Akithibitisha kuwepo kwa rushwa katijka vyombo vya habari wmandishi wa star tv abdalla pandu alisema imeshaanza kuota mizizi na hatua za dharura zinahitajika ili kuepusha madhara yanayoelekea kuikumba fani ya habari nchini.

“Waandishi tunapokea rushwa wakati mwengine kwa kujua au bila kujuana wengine wanaomba kabisa na kuchagua kazi za kwenda “ alisema mwandishi huyo na kuongeza kuwa hali hiyo sit u inapunguza heshima ya mwandishi na taaluma yake bali pia inaondoa wajibu wa mwandishi wa habari kwa jamii.

“Mwandishi ni kiyoo cha jamii na anatakiwa kuwa mfano bora kwao sasa inapotokea waandishi kunafanya kazi za ‘mishiko’ je zile za ‘makabwela’ wasio na pesa zitafanywa na nani?”, alihoji Pandu.

Mapema akiwasilisha muhtasari wa mada ya azimio la Dar es Salam juu ya uhuru uhariri na uwajibikaji, mwezeshaji Joyce Bazira alisema azimio hilo linatokana na mabadiliko yanayoikumba sekta ya habari yaliyoibua vitisho vingi katika ipatikanaji wa haki za msingi za binaadamu ikiwemo haki ya kupata habari na kujieleza.
  
Alisema kwa kutambua umuhimu wa vyombo vya habari na mabadiliko yanayoikuma sekta hiyo na wajibu wake kwa jamii ndipo azimio hilo likatolewa ili kuzingatia haja na mahitaji ya makundi yote ya kijamii.
katika kupiga vita suala hilo.

Akitoa mada kuhusiana na azimio hilo mkufuzi wa warsha hiyo maalim Juma Ali Simba alisema hali ya waandishi kuonesha uwajibikaji katika utendaji wa kazi zao ni jambo la lazima kwani bila ya maadili sekta hiyo haitaweza kufikia lengo la kuwa muhimili wa nne wa taifa.

Mafunzo hayo ya siku tatu yaliwashirikisha waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali vya Zanzibar  ikiwa ni hatua za Baraza la Habari Tanzania (MCT) katika kuwasilisha rasimu ya azimio hilo la Dar es saalam lililofikiwa mwaka uliopita.

No comments:

Post a Comment