Na: Mwinyimvua Nzukwi, Zanzibar
MIRADI YA MAENDELEO YA JAMII
Miradi mingi ya kijamii inayoanzishwa kupitia programu mbali mbali za
kitaifa zina lengo la kuinua hali za maisha ya wananchi, hivyo basi ipo haja
kwa wananchi hao kupewa fursa za kujadili, kupanga na hatimae kuanzisha miradi
hiyo kwa lengo la kuifanya kuwa endelevu na tija kwao na jamii kwa ujumla.
Hali ni tofauti katika sehemu nyingi nchini Tanzania na ukweli ni kwamba
miradi mingi imeibuliwa na ‘Waheshimiwa’ kwa lengo la kuwasaidia wananchi bali
unapotizamza kwa undani utagundua kuwa
miradi hiyo ni mitaji yao kisiasa na kupelekea miradi hiyo kufa na mengine
kusuasua bila ya kufikia malengo, kama ulivyo mradi huu wa ufugaji wa mbuzi wa
maziwa katika shehia ya Dole, Wilaya ya Magharibi, Mkoa wa Mjini Magharibi .
Pichani ni bi Fatma Bakari akiwa katika kutekeleza majukumu yake ya
kutafuta malisho kwa ajili ya mbuzi hao na picha ndogo akionesha mwenendo wa
mapato na matumizi yanayotokana na mradi huo ambapo ilibainika kuwa hakuna
uwiano kati ya gharama za uendeshaji za mradi huo na tija inayopatikana kiasi
cha kuwakatisha tamaa baadhi ya wanachama na kuamua kujitoa.
No comments:
Post a Comment