NAKAGUA:
Mnamo oktoba 28, 2012 Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alifanya ziara ya siku moja kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeleo iliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi na kufadhiliwa na serikali au washirika wa maendeleo.
Ziara hiyo ilihusisha vijiji vya Bweleo, Fumba na Bwefum viliopo wilaya ya Magharibi, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja. Haya ni baadhi ya matukio katika ziara hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia majengo
ya skuli ya Bwefum iliyoko Wilaya ya Magharibi, Mkoa wa Mjini Magharibi ambayo Mapaa yake yako katika hali ya uchakavu akiwa na
Mwalimu Mkuu wa Skuli hiyo Kesi Mwinyi Shomari pamoja na baadhi ya wanafunzi wa darasa la kwanza wa skuli hiyo.
Mwalimu mkuu wa skuli ya Bwefum, Kesi Mwinyi Shomari (wa kwanza kushoto aliyevaa kofia) akimuongoza Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi kukagua majengo na eneo la skuli hiyo siku kiongozi huyo alipotembelea vijiji vya Bweleo na Fumba kukagua miradi ya maendeleo na chanagamotozinazowakabili wananchi wa vijiji hivyo.
Mmiliki wa eneo lenye Magofu ya Bwefum, Bwana Chandra (wa kwanza kulia) akitoa maelezo kwaa Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi kufuatia mgogoro wa muda mrefu kati yake na Wananchi wa Kijiji Hicho. Balozi
Seif alizitaka pande hizo kuwa na subra wakati Serikali inafanya utafiti
utakaopelekea kupatikana kwa maamuzi sahihi ya kusuluhisha mgogoro huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi wa Uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu wa kijiji cha
Bweleo, Hassan Gharib (wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi juu ya changamoto wanazoipambana
nazo katika kutimiza azma yao. Wa kwanza kulia alievaa miwani ni mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Zanzibar (BTMZ) Sharifa Khamis.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifurahia bidhaa
zilizotengenezwa na Kikundi cha Ushirika cha Ukweli ni Njia Safi cha Kijiji cha
Bweleo. Kikundi hicho kinazalisha bidhaa mbali mbali za matumizi ya urembo na kawaida kwa kutumia mwani na mazao mengine ya baharini hali iliyomshawishi makamo huyo wa Rais kununua baadhi ya bidhaa hizo.
No comments:
Post a Comment