Monday, October 21, 2013

MISAADA YA EU IMECHACHUA MAENDELEO YA ZANZIBAR - MWINYIHAJI



Na Nwinyimvua Nzukwi

SERIKALI ya zanzibar imeelezea kuridhishwa kwake na misaada inayotolewa na Jumuiya ya Ulaya katika kuchochea maendeleo ya sekta mbali mbali na wananchi wa Zanzibar.

Akifungua mkutano wa majadiliano kuhusu mpango wa utekelezaji wa jumuiya hiyo kwa tanzania katka kipindi cha miaka 10 ijayo, kaimu waziri wa nchi afisi ya rais fedha na mipango ya maendeleo mheshimiwa mwinyihaji makame mwadini alisema misaada hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa katika ukuzaji wa uchumi wa Zanzibar kupitia mkakati wa kupunguza umaskini mkuza na mikakati mingine ya serikali.

Alisema toka jumuiya hiyo ianze kuisaisdia zanzibar mnamo mwaka 1990 sekta mbali mbali zimepata msukomo na kuchochea maendeleo ya jamii katika sekta mbali mbali zikiwemo  afya, sheria, elimu, uimarishaji wa miundo mbinu ya habari na mawasiliano na nishati.

“Toka tumeanza kupokea misaada ya jumuiya hii, kuna hatua kubwa za kimaendeleo zimefikiwa ikiwemo kupunguza kasi ya ueneaji wa maradhi kujamiana, kupunguza umaskini wa kipato na mradi wa kupambana na ajira za watoto na ukatili wa kijinsia uliotekelezwa katii ya mwaka 1995 na 2000 ikiwa ni sehemu ya mkuza awamu ya kwanza ”, alisema mheshimiwa Dk. Mwinyihaji.

Nae balozi wa jumuhiya  hiyo nchini Tanzania Mheshimiwa filiberto Cerian Sebrigondi aliwataka washiriki wa mkutano huo kutumia mkutano kufungua majadiliano kwa ajili ya ufadhili wa miradi ya maendeleo inayotarajiwa kufadhiliwa na jumuiya yake katika kipindi cha kuazia mwaka 2014 hadi 2020.

“Kimsingi umoja wa ulaya unaridhisha na matumizi ya misaada inayotolewa kwa tanzania na ni vyema mkatumia mkutano huu kufungua majadiliano juu ya miradi tunayotarajia kuisaidia katika kipindi kijacho”, alisema balozi huyo.

Alisema kuwa katika utekelezaji wa mradi mpango huo msukazo mkubwa utawekwa katika kuimarisha sekta za utawala bora, nishati na kilimo kama yalivyo katika mipango ya taifa ya MKUKUTA na MKUZA.

Akifafanua namna ya utekelezaji wa mpango huo, mkuu wa kitengo cha ushirikiano wa umoja huo nchini Eric Beaume alisema sekta hizo zimechaguliwa kutokana na kuwa na mchango mkubwa na wa moja kwa moja katika maisha ya maisha ya wananchi jambo ambalo litasaidia kukuza uchumi wao na kupunguza umaskini miongoni mwa jamii.
“katika kuimarisha utawala bora, kuimarisha kilimo kuwa cha kisasa na upatikanaji wa nishati ya uhakika tunaamini kutachochea zaidi kasi ya maendeleo ya jamii na kuzisaidia serikali kutimiza wajibu wake”, alisema Beaume.

Wakichangia mada zilizowasilishwa kuhuhusu utekelezaji huo kwa nyakati tofauti rais wa jumuiya ya wafanyabiashara wenye viwanda na wakulima abdallah omar na mkurugenzi wa shirika la mfuko wa Agakhan, khamis abdalla said waliitaka jumuiya hiyo kuzingatia ushirikishwaji wa sekta binafsi katka upangaji na utekelezaji wa miradi inayoihusu jamii ili kutoa matokeo yaliyobora zaidi.

“Ni vyema sasa EU ikazingatia ushirikishwaji wa sekta binafsi zinazojihusisha na kutoa huduma kwa jamii katika nyanja tofauti ili kuwasaidia kuimarisha hali za maisha kwa kiwango kilicho bora zaidi”, alisema saidi akitolea mfano mkakati wa jumuiya hiyo katika kukuza kilimo endelevu kupitia mipango ya kilimo kwanza unaotekelezwa tanzania bara na mapinduzi ya kijani wa zanzibar.

 Aidha waliipongeza jumuiya hiyo na serikali za tanzania kwa juhudi wanazochukua katika kutatua kero za wananchi na kuwaletea maendeleo.

Mkutano huo wa siku moja uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Grand palace, Malindi ulikuwa maalum katika kujadili


No comments:

Post a Comment