WAKANDARASI WATAKIWA KUZINGATIA UTAALAMU, VIWANGO
UJENZI WA BARABARA
Na Mwinyimvua Nzukwi,
Zanzibar
KAMPUNI na wataalamu wa ujenzi wa barabara nchini
wametakiwa kuhakikisha wanazingatia utaalam ili kuzifanya barabara hizo kuwa katika kiwango kinachokubakila Kimataifa na
zinadumu kwa muda mrefu.
Wito huo umetolewa na
makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar balozi seif ali iddi alipofanya ziara ya
kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Jendele – Cheju - Kaebona yenye
urefu wa kilomita 11.7 unaofanywa na kampuni ya D.P Shapriya +Co. Ltd ya Dara
es salaam ambayo ni miongoni mwa bara
bara iliyomo katika mradi wa ujenzi wa bara bara tatu za vijijini katika kisiwa
cha Unguja.
Alisema serikali
inatambua kuwepo kwa wahandisi na wasimamizi wa ujenzi wa barabara wasio waaminifu
ambao baadhi ya wakati hufanya kazi kwa kuondoa njiani miradi wanayopewa bila
ya kuzingatia masharti na mikataba ya ujenzi.
Alisema hali hiyo
huleta kero kwa wafadhili wa miradi na wakati mwengine kuyatia hasara mataifa yenye
miradi hiyo ambayo yanayoshindwa kuihudumia na kuiendeleza miradi husika
kutokana na ufinyuna ukuwaji mdogo wa uchumi wa nchi zao.
“Baadhi ya makandarasi
wamekuwa na tabia ya kuondosha njiani kazi wanazopewa tabia ambayo huwakera wafadhili na kwa upande
mwengine kuyaongezea mzigo mataifa yenye kusaidiwa ufadhili wa miradi hiyo”, alisema
Balozi Seif.
Akizungumzia suala la
fidia kwa vipando na mali za wananchi walioathirika na miradi hiyo, Makamo huyo
wa Rais aliiagiza Wizara ya Miundo Mbinu na Mawasiliano Zanzibar kufanya
upembuzi yakinifu ili kuepukana na baadhi ya watu wajanja wenye tabia ya
kujipandikiza katika madai ya fidia na kuwakosesha haki watu wanaohusika jambo
ambalo amedai kuwa ni chanzo cha migogoro kati yao na serikali.
“Kuna tabia imekuwa
ikijichomoza mara kwa mara wakati wa uanzishwaji wa miradi kama hii kwa baadhi
ya watu wasiohusika kudai fidia katika maeneo mbali mbali nchini na kuitia
hasara serikali kwa vile wanakuwa hawamo katika jabeti iliyokubalika kabla ya
kuanza kwa mradi na kuisababishia hasara serikali na kupunguza kasi ya
utekelezaji wa miradi hiyo hivyo ni vyema mkawa makini zaidi”, alisistiza.
Aidha Balozi Seif aliipongeza
kampuni ya D.P Shapriya +Co. Ltd ya Dara es salaam inayonga barabara hiyo kwa
hatua iliyofikia katika utekelezaji wa mradi huo licha ya kuchelewa kutokana na
mvua za masika jambo ambalo linatia moyo ya kuweza kukamilika kwa mradi huo
katika muda uliopangwa.
Mapema Msimamizi wa
Mradi huo Wizara ya Miundo Mbinu na Mawasiliano Zanzibar, Mhandisi Suleiman
Abdulla Ali alisema serikali kupitia wizara husika tayari imeshawalipa fidia
wananchi wote waliohusika katika mradi huo na kwamba tathmini imeshafanywa kwa ajili ya waathiria wa mradi
wa barabara ya Koani – Jumbi yenye urefu wa Kilo Mita 6.3 na wizara husika italipa fidia mara tuu fedha
zitakapopatikana.
Aidha alifahamisha kuwa
kutokana na ufinyu wa bajeti ya kazi za ujenzi wa barabara hizo umepelekea
kutolewa kwenye mradi huo ujenzi wa barabara ya Kizimbani hadi Kiboje yenye urefu
wa kilomita 7.
Akitoa maelezo ya
utekelezaji wa miradi hiyo Mshauri muelekezi wa Mradi huo kutoka kampuni ya
Newtech Consulting Group ya Sudan, El-Tayeb Rabah Mohammed alisema kuwa mradi
huo umepangwa kuchukuwa miezi 17 hadi
kukamilika kwake mnamo mwezi Mei mwakani.
El – Tayeb
alimuhakikishia Balozi Seif kwamba ana matumaini ya kupatikana na kukamilika
kwa ujenzi huo kwa kiwango kizuri
kitakachokidhi mahitaji yaliyokusidiwa kwa pande zote mbili.
Alieleza kuwa
Wataalamu hao wa ujenzi wameshasafisha eneo la wastani wa kilomita 10 hadi sasa
na kufanya kazi za kutengeneza tabaka la chini kwa wastani wa kilomita 2 kwa
Bara bara ya Cheju –Jendele – Kaebona.
Mkataba kati wa
utekelezaji wa mradi huo kati ya SMZ kupitia wzara ya miundombinu na
mawasiliano na Kampuni ya DP Shapriya + Co Ltd ya Dar es salaam kwa kazi za
utekelezaji mnamo tarehe 11 Septemba mwaka 2012na ujenzi wa kazi hiyo kuanza
mapema Januari mwaka huu umegharamiwa na Benki ya Maendeleo ya Kiislamu (BADEA)
kwa kushirikiana na SMZ ambapo zaidi cha shilingi za kitanzania bilioni 14.8
zitatumika .
Kukamilika kwa barabara
hizo inatarajiwa kupunguza kwa kiasi tatizo la usafiri kwa wakulima wa zao la
mpunga katika bonde la Cheju ambao walikuwa wakipata usumbufu kwa miaka kadhaa
sasa wakati wa kusafirisha mazao na kuwaunganisha wanachi wa maeneo ya wilaya ya kati na kusini Unguja kwa unafuu.
No comments:
Post a Comment