·
MALINZI RAIS MPYA TFF,
ATANGAZA MSAMAHA KWA WOTE WALIOADHIBIWA NA
KAMATI YA TENGA
Katika hali inayotafsiriwa kama kuweka mambo sawa ndani ya tff
na soka la Tanzania, rais mpya wa shirikisho la soka Tanzania, jamali malinzi
ametoa msamaha kwa viongozi na wadau mbali mbali wa mchezo huop walioadhibiwa
na kamati iliyopita.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi
uliomalizika usiku wa kuamkia Jumatatu ya Oktoba 28 katika ukumbi wa NSSF Water
Front, Dar es Salaam, Malinzi aliiagiza Sekretarieti ya TFF chini ya Katibu wake,
Angetile Osiah kuandika barua za misamaha kwa watu wote wanaotumikia adhabu za
utawala wa Tenga.
“Hata Rais wa nchi anapoingia madarakani huwa anatoa misamaha, nami nachukua fursa hii kuomba ridhaa yenu wajumbe wenzangu, kwa kuwa huu ni uongozi mpya, basi tufungue ukurasa mpya, nipeni ridhaa yenu, watu wote waliofungiwa chini ya utawala uliomaliza muda wake, wasamehewe tuanze upya, isipokuwa wale tu ambao adhabu zao zinatokana na rushwa na upangaji matokeo,”alisema Malinzi.
Malinzi alisema muda si mrefu atakutana na Kamati tendaji kujipanga na kuwataka wajumbe wote kujiandaa kwa hilo.
Kwa upande wake, Rais aliemaliza muda wake Leodga Chilla Tenga alimpongeza rais huyo mwenye historia kubwa katika michezo na kuahidi kumkabidhi ofisi mapema Jumamosi ijayo ili kuendelea na majukumu yake.
Malinzi alishinda kushika nafasi hiyo baada kupata kura 72,
dhidi ya 52 za mpinzani wake Athumani Jumanne Nyamlani.
aidha Walace Karia alifanikiwa kushinda nafasi ya Makamu wa Rais baada ya kupata kura 67 na kuwashinda makamo wa rais katika kamati iliyomaliza muda wake Nassib Ramadhani aliyepata kura 52 na mwenekiti wa zamani wa klabu ya yanga Imani Madega aliyeambulia kura 6.
Katika nafasi za Ujumbe kutoka kanda ya13, kiungo wa zamani wa klabu ya Simba SC Wilfred Kidau alipata kura 60 na kuwashinda Muhsin Said (50), mwamuzi mwandamizi Omar Abdulkadir (10) na Alex Kabuzelia (4).
Kanda ya 12 mshindi alikuwa ni Khalid Mohamed Abdallah aliepata kura 69 na kumshinda Davisa Mosha aliyepata kura 54 huku katika Kanda ya 11 makamo mwenyekiti wa zamani wa samba s. c Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ akishinda kwa kura 78 na kuwashinda Riziki Majala aliyepata kura 5, Twahir Njoki kura 2, mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto kura 26 na Farid Mbaraka kura 14.
Katika uchaguzi huo uliovuta hisia za wengi kutokana na
kushindwa kufanyika katika siku za nyuma hadi kupelikea shirikisho la mpira wa
miguu ulimwenguni FIFA kuingilia kati, ulishuhudia Hussein Mwamba akiwa mshindi
toka kanda ya 10 kwa kupata kura 63 dhidi ya Charles Komba aliyepata kura 4 na
Stewart Nasima aliyepata kura 58.
Kanda ya 9 itawakilishwa na Othman Kambi aliyepata kura 84 baada ya kumshinda Francis Bulame aliyepata kura 30 wakati James Mhagama aliyemshinda Zafarani Damoda kwa kura 93 dhidi ya kura 11 na kuingia katika ofisi hizo kuiwakilisha kanda ya 8, wakati Vedastus Lufano aliyepata kura 51, amewashinda Jumbe Odesa Magati (kura 11), Mugisha Galibona (kura 24) na Samuel Nyalla (kura 39) katika kanda ya 7.
Katika kanda ya 6 mshindi ni Ngube Kiondo aliyepata kura 73 na
kumshinda Ayoub Nyaulingo kura 52 wakati katika
Kanda ya 5, Ahmed Iddi Mgoyi alishinda kwa kupata kura 92 dhidi ya Yussuf Kitumbo aliyepata kura 34 na Omar Walii Ali wa kanda ya 4 alishinda kwa kura 53 dhidi ya 19 za Ally Mtumwa.
Kanda ya 5, Ahmed Iddi Mgoyi alishinda kwa kupata kura 92 dhidi ya Yussuf Kitumbo aliyepata kura 34 na Omar Walii Ali wa kanda ya 4 alishinda kwa kura 53 dhidi ya 19 za Ally Mtumwa.
Uchaguzi huo uliosimamiwa kikamilifu na wakili machachari Hamid Mbwezeleni pia Eley Mbise alishinda ujumbe wa kamati tendaji kutoka kanda ya 3 baada ya kwa kupata kura 51 dhidi ya 53 za Lamanda Swai huku Mbasha Matutu aliyepata kura 63 akimbwaga Vesastis Ligano aliyepata kura 61 katika Kanda ya 2 wakati kanda ya kwanza Karilo Samson alitawazwa kuwa mshindi bila ya kupigiwa kura baada ya kutokuwa na mpizani.
Malinzi mwenye umri wa miaka 52 sasa ni rais wa pili toka kufanyike
mabadiliko ya muundo wa taasisi hiyo inayosimamia soka nchini Tanzania kutoka
chama cha mpira kilichojulikana kama FAT hadi mfumo wa sasa wa shirikisho.