Monday, October 28, 2013

MALINZI RAIS MPYA TFF

·  
MALINZI RAIS MPYA TFF,
 ATANGAZA MSAMAHA KWA WOTE WALIOADHIBIWA NA KAMATI YA TENGA

Katika hali inayotafsiriwa kama kuweka mambo sawa ndani ya tff na soka la Tanzania, rais mpya wa shirikisho la soka Tanzania, jamali malinzi ametoa msamaha kwa viongozi na wadau mbali mbali wa mchezo huop walioadhibiwa na kamati iliyopita.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi uliomalizika usiku wa kuamkia Jumatatu ya Oktoba 28 katika ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam, Malinzi aliiagiza Sekretarieti ya TFF chini ya Katibu wake, Angetile Osiah kuandika barua za misamaha kwa watu wote wanaotumikia adhabu za utawala wa Tenga.

“Hata Rais wa nchi anapoingia madarakani huwa anatoa misamaha, nami nachukua fursa hii kuomba ridhaa yenu wajumbe wenzangu, kwa kuwa huu ni uongozi mpya, basi tufungue ukurasa mpya, nipeni ridhaa yenu, watu wote waliofungiwa chini ya utawala uliomaliza muda wake, wasamehewe tuanze upya, isipokuwa wale tu ambao adhabu zao zinatokana na rushwa na upangaji matokeo,”alisema Malinzi.

Malinzi alisema muda si mrefu atakutana na Kamati tendaji kujipanga na kuwataka wajumbe wote kujiandaa kwa hilo.

Kwa upande wake, Rais aliemaliza muda wake Leodga Chilla Tenga alimpongeza rais huyo mwenye historia kubwa katika michezo na kuahidi kumkabidhi ofisi mapema Jumamosi ijayo ili kuendelea na majukumu yake. 

Malinzi alishinda kushika nafasi hiyo baada kupata kura 72, dhidi ya 52 za mpinzani wake Athumani Jumanne Nyamlani.

aidha Walace Karia alifanikiwa kushinda nafasi ya Makamu wa Rais baada ya kupata kura 67 na kuwashinda makamo wa rais katika kamati iliyomaliza muda wake Nassib Ramadhani aliyepata kura 52 na mwenekiti wa zamani wa klabu ya yanga Imani Madega aliyeambulia kura 6.
   
Katika nafasi za Ujumbe kutoka kanda ya13, kiungo wa zamani wa klabu ya Simba SC Wilfred Kidau alipata kura 60 na kuwashinda Muhsin Said (50), mwamuzi mwandamizi Omar Abdulkadir (10) na Alex Kabuzelia (4).

Kanda ya 12 mshindi alikuwa ni Khalid Mohamed Abdallah aliepata kura 69 na kumshinda Davisa Mosha aliyepata kura 54 huku katika Kanda ya 11 makamo mwenyekiti wa zamani wa samba s. c Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ akishinda kwa kura 78 na kuwashinda Riziki Majala aliyepata kura 5, Twahir Njoki kura 2, mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto kura 26 na Farid Mbaraka kura 14.
Katika uchaguzi huo uliovuta hisia za wengi kutokana na kushindwa kufanyika katika siku za nyuma hadi kupelikea shirikisho la mpira wa miguu ulimwenguni FIFA kuingilia kati, ulishuhudia Hussein Mwamba akiwa mshindi toka kanda ya 10 kwa kupata kura 63 dhidi ya Charles Komba aliyepata kura 4 na Stewart Nasima aliyepata kura 58.

Kanda ya 9 itawakilishwa na Othman Kambi aliyepata kura 84 baada ya kumshinda Francis Bulame aliyepata kura 30 wakati James Mhagama aliyemshinda Zafarani Damoda kwa kura 93 dhidi ya kura 11 na kuingia katika ofisi hizo kuiwakilisha kanda ya 8, wakati Vedastus Lufano aliyepata kura 51, amewashinda Jumbe Odesa Magati (kura 11), Mugisha Galibona (kura 24) na Samuel Nyalla (kura 39) katika kanda ya 7.
Katika kanda ya 6 mshindi ni Ngube Kiondo aliyepata kura 73 na kumshinda Ayoub Nyaulingo kura 52 wakati katika
Kanda ya 5, Ahmed Iddi Mgoyi alishinda kwa kupata kura 92 dhidi ya Yussuf Kitumbo aliyepata kura 34 na  Omar Walii Ali wa kanda ya 4 alishinda kwa kura 53 dhidi ya 19 za Ally Mtumwa. 

Uchaguzi huo uliosimamiwa kikamilifu na wakili machachari Hamid Mbwezeleni pia Eley Mbise alishinda ujumbe wa kamati tendaji kutoka kanda ya 3 baada ya kwa kupata kura 51 dhidi ya 53 za Lamanda Swai huku Mbasha Matutu aliyepata kura 63 akimbwaga Vesastis Ligano aliyepata kura 61 katika Kanda ya 2 wakati kanda ya kwanza  Karilo Samson alitawazwa kuwa mshindi bila ya kupigiwa kura baada ya kutokuwa na mpizani.


Malinzi mwenye umri wa miaka 52 sasa ni rais wa pili toka kufanyike mabadiliko ya muundo wa taasisi hiyo inayosimamia soka nchini Tanzania kutoka chama cha mpira kilichojulikana kama FAT hadi mfumo wa sasa wa shirikisho.

Monday, October 21, 2013

SMZ KUVISAIDIA VYOU VYA AMALI VINAVYOZALISHA AJIRA


Na. Othman Khamis, OMKPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema nia ya Serikali  ya kuanzisha wizara inayosimamia  sekta  ya kazi  ni  kuhakikisha kwamba inapambana na tatizo la ajira linaloonekana kuathiri nguvu kubwa ya vijana nchini. 

Kauli hiyo aliitoa wakati  akizindua Chuo cha Ushoni na ujasiriamali  kilichoanzishwa na  Jumuiya ya Vijana ya Kibweni  ya Kibweni Yourth Organization KYO iliyopo Kibweni kwa Botoro,Jimbo la Bububu, wilaya ya Magharibi Unguja.

Alisema hatua hiyo pia inakwenda sambamba na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayoelezea umuhimu wa kuundwa  kwa vikundi vya  ujasiri amali ambavyo hutoa fursa ya ajira miongoni mwa wananchi.

Alisema kazi hizo zimekuwa zikisaidia kupunguza umaskini  na serikali itajitahidi kuhakikisha inavijengea nguvu vikundi hivyo vya ili viweze kutekeleza majukumu vilivyojipangia.

Aidha aliipongeza jumuiya hiyo kwa uamuzi  wa kuanzisha kikundi hicho ambacho kinatarajiwa kuwa mkombozi kwa wanajumuiya na vijana wa jimbo hilo kwa ujumla.
Balozi Seif aliwahimiza viongozi na wana jumuiya hiyo kuwa wastahamilivu na kuvumiliana katika harakati zao za kila siku hatua ambayo itafanikiwa endapo kutakuwa na  utaratibu wa kufuata kanuni walizojiwekea.

“ Nimefurahi kuona vijana mmejikusanya kuanzisha mfumo wa ajira ambao serikali kuu kadri ya hali itakavyoruhusu itazingatia na kutoa msaada unaostahiki ili kukiendeleza kikundi chenu”, alisisitiza Balozi Seif.

Aliwahimiza kuendelea na mpango waliouanzisha wa kupanda miti ili kukabiliana na upungufu wa maji uliyoikumba nchi kutokana na tabia za baadhi ya watu kukata miti ovyo.

Katika kuunga mkono juhudi za vijana hao za kuanzisha chuo hicho Makamu huyo wa Rais alikabidhi vyarahani vitano kama mchango wake katika kukipa nguvu chuo hicho.
Vile vile aliahidi kuchangia kompyuta moja na mashine ya kudarizi kwa chuo hicho hatua  ambayo imeungwa mkono na Mwakilishi wa jimbo hilo Hussein Ibrahim Makungu ‘BHAA’ aliyetoa mchango wa shilingi Milioni 2 wakati Mbunge wa Jimbo hilo Masoud Sururu ambaye ni mlezi wa jumuiya hiyo akIahidi kuchangia vyarahani vitano, pasi na vifaa vingine vidogo vidogo. 

Akisoma  risala kwa niaba ya wanajumiya wenzake Farida Juma Haji alisema vijana wa Kibweni wameamua kuanzisha  jumuiya hiyo wakitambua kwamba serikali kuu haina fursa ya kutoa ajira kwa watu wote.

Alisema elimu ya ujasiri amali ambayo ni muhimu kwa taifa lolote Duniani ndio itakayowapa nafasi pekee ya kukabiliana na tatizo la ajira na kwamba jumuiya yao  imelenga kwenda sambamba na mpango wa taifa wa kupunguza umaskini Zanzibar (MKUZA).

Mapema akikikagua chuo hicho Mwalimu  wa chuo hicho Subira Haji Yahya alimueleza Balozi Seif kwamba lengo la kuanzishwa kwa chuo hicho ni kuwajengea mazingira ya ajira vijana wa Shehia hiyo.

Subira alieleza kwamba mfumo huo wa mafunzo mbali ya kutengeneza kazi za ajira lakini pia utasaidia kupunguza wimbi la vitendo viovu wanavyojihusisha zaidi vijana ndani ya mitaa na kuleta kero na fadhaa kwa jamii.

Chuo cha ushoni cha ujasiri amali cha Kwa Botoro kilichoanzishwa takribani miezi tisa iliyopita kina wanafunzi 16 wa rika mbali mbali ambao mbali ya kujifunza ushonaji wa nguo kwa hatua mbali mbali pioa hupata wasaa wa kujifunza lugha ya Kiingereza pamoja na upandaji miti katika maeneo ya vianzio vya maji vya Mwanyanya.


JESHI LA BAUSI



BAUSI ATAJA NYOTA WA CHALLENJI

Na. Mwinyimvua Nzukwi, Zanzibar
  


Na. Mwinyimvua Nzukwi, Zanzibar
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’, Salum Bausi amewaita nyota 30 kuunda kikosi cha timu hiyo kinachojiandaa na michuano ya Chalenji inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mjini Nairobi Kenya baadae mwaka huu.



Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa uwanja wa Amaan mjini hapa, Bausi alisema pamoja na kuwaona wachezaji wengi katika ligi madaraja tofauti ya hapa Zanzibar na wale wanaoshiriki ligi kuu ya Tanzania bara, amezingatia mambo makubwa manne ili kuipata timu hiyo.

Aliyataja mambo hayo kuwa ni nidhamu ya mchezaji, uwezo wa mchezaji binafsi, nafasi ya mchezaji katika timu yake na ukubwa wa mashindano wanayojiandaa nayo jambo ambalo amesema litawapa nafasi wachezaji hao kuongeza juhudi na kujituma wakiwa katika timu hiyo.
“Pamoja na mambo yote hayo mkazo mkubwa kwangu ni katika nidhamu ya mchezaji, ndani na nje ya uwanja kwani naamini ni vigumu kama mwalimu kuwa na timu yenye matokeo mazuri bila ya wachezaji wanaozingatia nidhamu wakati wote”, alisema Bausi.

 Bausi ambaye awali alitangaza kujiuzulu timu kuifundisha timu hiyo mara baada ya kushika nafasi ya tatu katika mashindano yaliyopita yaliyofanyika Kampala, Uganda na alirudishiwa jukumu hilo na ZFA (chama cha soka Zanzibar) baada ya kushauriwa wa Rais wa Zanzibar Dk. Ali mohammed Shein. Aliwataka wadau wa mchezo huo kujitokeza na kumpa ushirikiano na kwamba yeye atakua tayari kupokea ushauri wowote ule.

“Hii timu hii si yangu wala ZFA ni yetu sote, sasa kila mmoja anaruhusiwa kutoa mchango, maoni, ushauri na kila aina ya msaada ambao anahisi utasaidia katika kuleta matokeo mazuri ya timu hii”, aliongeza.

Wachezaji watakaounda timu hiyo na timu zao kwenye mabano ni walinda milango Mwadini Ali Mwadini (Azam fc), Abdalla Rashid ‘Babu’ (Ruvu Shooting) na Ali Suleiman Abdi (KMKM) wakati walinzi ni Mohammed Azan ‘Brown’ (Polisi - Zanzibar), Waziri Salum (Azam ), Shafii Hassan (Malindi) na Mohammed Faki (Zimamoto).

Wengine katika nafasi hiyo ni Salum Haji Juma (Miembeni), Said Yussuf (Mtende Rangers), Mohammed Othman Mmanga (Jamhuri), Mussa Said Magarawa (Chwaka Stars) na Nassor Masoud ‘Cholo’ (Simba).

Viungo wa timu hiyo ni pamoja na Abdulhalim Humuod (Simba), Sabri Ali Makame (Oljoro JKT), Adeyoum Saleh (Simba) na Is-haka Othman (JKU).

Wengine ni Ali Kani Mkanga (JKT Ruvu), Hamadi Mshamata (Chuoni), Hamadi Juma Issa  na Masoud Ali Mohammed (Mtibwa Sugar).

Washambuliaji katika kikosi hicho kinachotarajiwa kuanza mazoezi Alhamisi ijayo baada ya kukamilika kwa zoezi la upimaji wa afya siku ya Jumatano ni Seif Abdalla Rashid na Khamis Mcha Khamis ‘Viali’ wa Azam, Suleiman Kassim Suleiman ‘Solembe’ (Coastal Union), Amour Omar Mohammed ‘Janja’ (Miembeni) na Amir Omar Hamad (Oljoro JKT).

Wachezaji wengine katika safu ya ushambuliaji ni Jaku Joma Jaku (Mafunzo), Faki Nahoda (Kimbunga F. C), Hassan Seif Ali (Mtibwa)  na mfungaji bora wa mashindano ya kombe copa cola yaliyomalizika hivi karibuni Juma Ali Yussuf  anaechezea timu ya New Vission inayoshiriki ligi daraja la central wilaya ya Mjini, Unguja.

Akizungumzia uteuzi huo mjumbe wa Kamati Tendaji ya ZFA Taifa Maalim Masoud Attai aliwataka wapenzi wa mpira wa miguu visiwani hapa wakubaliane nao kutokana na kuwa umezingatia vigezo vya kitaaluma na waisaidie ili kuwatia moyo wachezaji na viongozi wa timu hiyo.

“Huu ni uteuzi wa mwalimu na wenzake na sisi sote hatuna budi kuunga mkono kwa sababu wao ndio tuliwakabidhi kazi hivyo ni vyema tukawasaidia kutekeleza majukumu yao”, alisema Maalim Attai.

Timu hiyo ambayo inatarajiwa kucheza mechi mbali mbali za mchujo ili kupata wachezaji 20 watakaoenda Nairobi, ipo chini ya Bausi anayesaidiwa na Hafidh Muhidin na Malale Hamsini huku Saleh Ahmed Seif akipewa jukumu la kuwanoa makipa wa timu hiyo na daktari wa timu ni Mohammed Mwinyi na mtunza vifaa (kit manager) ni Mohammed Said ‘Mdudu’.

MISAADA YA EU IMECHACHUA MAENDELEO YA ZANZIBAR - MWINYIHAJI



Na Nwinyimvua Nzukwi

SERIKALI ya zanzibar imeelezea kuridhishwa kwake na misaada inayotolewa na Jumuiya ya Ulaya katika kuchochea maendeleo ya sekta mbali mbali na wananchi wa Zanzibar.

Akifungua mkutano wa majadiliano kuhusu mpango wa utekelezaji wa jumuiya hiyo kwa tanzania katka kipindi cha miaka 10 ijayo, kaimu waziri wa nchi afisi ya rais fedha na mipango ya maendeleo mheshimiwa mwinyihaji makame mwadini alisema misaada hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa katika ukuzaji wa uchumi wa Zanzibar kupitia mkakati wa kupunguza umaskini mkuza na mikakati mingine ya serikali.

Alisema toka jumuiya hiyo ianze kuisaisdia zanzibar mnamo mwaka 1990 sekta mbali mbali zimepata msukomo na kuchochea maendeleo ya jamii katika sekta mbali mbali zikiwemo  afya, sheria, elimu, uimarishaji wa miundo mbinu ya habari na mawasiliano na nishati.

“Toka tumeanza kupokea misaada ya jumuiya hii, kuna hatua kubwa za kimaendeleo zimefikiwa ikiwemo kupunguza kasi ya ueneaji wa maradhi kujamiana, kupunguza umaskini wa kipato na mradi wa kupambana na ajira za watoto na ukatili wa kijinsia uliotekelezwa katii ya mwaka 1995 na 2000 ikiwa ni sehemu ya mkuza awamu ya kwanza ”, alisema mheshimiwa Dk. Mwinyihaji.

Nae balozi wa jumuhiya  hiyo nchini Tanzania Mheshimiwa filiberto Cerian Sebrigondi aliwataka washiriki wa mkutano huo kutumia mkutano kufungua majadiliano kwa ajili ya ufadhili wa miradi ya maendeleo inayotarajiwa kufadhiliwa na jumuiya yake katika kipindi cha kuazia mwaka 2014 hadi 2020.

“Kimsingi umoja wa ulaya unaridhisha na matumizi ya misaada inayotolewa kwa tanzania na ni vyema mkatumia mkutano huu kufungua majadiliano juu ya miradi tunayotarajia kuisaidia katika kipindi kijacho”, alisema balozi huyo.

Alisema kuwa katika utekelezaji wa mradi mpango huo msukazo mkubwa utawekwa katika kuimarisha sekta za utawala bora, nishati na kilimo kama yalivyo katika mipango ya taifa ya MKUKUTA na MKUZA.

Akifafanua namna ya utekelezaji wa mpango huo, mkuu wa kitengo cha ushirikiano wa umoja huo nchini Eric Beaume alisema sekta hizo zimechaguliwa kutokana na kuwa na mchango mkubwa na wa moja kwa moja katika maisha ya maisha ya wananchi jambo ambalo litasaidia kukuza uchumi wao na kupunguza umaskini miongoni mwa jamii.
“katika kuimarisha utawala bora, kuimarisha kilimo kuwa cha kisasa na upatikanaji wa nishati ya uhakika tunaamini kutachochea zaidi kasi ya maendeleo ya jamii na kuzisaidia serikali kutimiza wajibu wake”, alisema Beaume.

Wakichangia mada zilizowasilishwa kuhuhusu utekelezaji huo kwa nyakati tofauti rais wa jumuiya ya wafanyabiashara wenye viwanda na wakulima abdallah omar na mkurugenzi wa shirika la mfuko wa Agakhan, khamis abdalla said waliitaka jumuiya hiyo kuzingatia ushirikishwaji wa sekta binafsi katka upangaji na utekelezaji wa miradi inayoihusu jamii ili kutoa matokeo yaliyobora zaidi.

“Ni vyema sasa EU ikazingatia ushirikishwaji wa sekta binafsi zinazojihusisha na kutoa huduma kwa jamii katika nyanja tofauti ili kuwasaidia kuimarisha hali za maisha kwa kiwango kilicho bora zaidi”, alisema saidi akitolea mfano mkakati wa jumuiya hiyo katika kukuza kilimo endelevu kupitia mipango ya kilimo kwanza unaotekelezwa tanzania bara na mapinduzi ya kijani wa zanzibar.

 Aidha waliipongeza jumuiya hiyo na serikali za tanzania kwa juhudi wanazochukua katika kutatua kero za wananchi na kuwaletea maendeleo.

Mkutano huo wa siku moja uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Grand palace, Malindi ulikuwa maalum katika kujadili