WAANDISHI WATAKA AZIMIO LIWAFIKE WADAU WOTE
Na
Mwinyimvua Nzukwi, Zanzibar
Waandishi wa
habari nchini walitaka baraza la habari Tanzania kuendelea kulielimisha wadau
mbali mbali wa sekta ya habari juu ya azimio la Dar es salaam kuhusu uhuru wa
uhariri na uwajibikaji wa wadau wanaochangia uanzishwaji na uendeshaji wa
vyombo vya habari.
Wakichangia
mada washiriki wa mafunzo ya siku tatu kuhusu maadili ya vyombo vya habari
wamesema wamiliki, wafanyabiashara na wanasiasa wanachangia wamekuwa
wakandamizaji na wavunjaji wakubwa wa maadili ya uandishi na waandishi wa
habari jambo linalochochea kuporomoka hadhi ya taaluma ya habari.
“Pamoja na
uzuri wa mafunzo haya kwetu lakini ni vyema baraza likawafanyia na wamiliki wa
vyombo tunavyofanyia kazi labda inaweza kupunguza kasi ya ukiukwaji ya maadili
yqa fani yetu”, alisema Suzan Kunambi.
Kunambi
ambaye pia ni katibu mtendaji wa Zanzibar Press Club alisema suala la maadili
ndio msingi wa taaluma na waandishi wanajitahidi kufungamana nalo ila wamiliki
na wadau wengine huwa ndio tatizo linalowafanya waandishi kutokuwa na hiyari
katika kutii ammri za mabosi wao.
“Utakuta
wakati jambo unalijua kuwa ni kinyume na utaratibu, unamwambia mkubwa wako kuwa
hivi sivyo lakini anakwambia fanya ninavyotaka, na ukiangalia una njaa ya kazi
basi unalazimika kutii japo kwa shingo upande”, aliongeza katibu huyo.
Naye zaituni
makwali mwandishi wa kituo cha redio cha chuchu fm alisema kuwasilishwa kwa
asimio hilo kwa wadau wote kutasaidia kuongeza uelewa na uwajibikaji wa sekta
hiyo kwa maslahi ya jamii na taifa kwa ujumla.
Alisema
hatua hiyo itasaidia kupunguza wamesikitishwa na vitendo vya rushwa na
upendeleo vinavyoendelea kushamiri katika vyombo vya habari kiasi cha kuwa
chanzo cha migogoro miongoni mwa waandishi.
“Utamkuta
mkubwa Fulani katika chombo ana urafiki na mtu mwengine sasa anakitumia chombo
chake kumpendelea rafiki yake au taasisi yake bila ya kutoa fursa ya mtu
mwengine kujitetea, sasa mambo kama haya yanahitaji kuchukuliwa hatua za haraka
ili kuzuia mfarakano katika jamii”, alisema.
Akithibitisha
kuwepo kwa rushwa katijka vyombo vya habari wmandishi wa star tv abdalla pandu
alisema imeshaanza kuota mizizi na hatua za dharura zinahitajika ili kuepusha
madhara yanayoelekea kuikumba fani ya habari nchini.
“Waandishi
tunapokea rushwa wakati mwengine kwa kujua au bila kujuana wengine wanaomba
kabisa na kuchagua kazi za kwenda “ alisema mwandishi huyo na kuongeza kuwa
hali hiyo sit u inapunguza heshima ya mwandishi na taaluma yake bali pia
inaondoa wajibu wa mwandishi wa habari kwa jamii.
“Mwandishi
ni kiyoo cha jamii na anatakiwa kuwa mfano bora kwao sasa inapotokea waandishi
kunafanya kazi za ‘mishiko’ je zile za ‘makabwela’ wasio na pesa zitafanywa na
nani?”, alihoji Pandu.
Mapema
akiwasilisha muhtasari wa mada ya azimio la Dar es Salam juu ya uhuru uhariri
na uwajibikaji, mwezeshaji Joyce Bazira alisema azimio hilo linatokana na
mabadiliko yanayoikumba sekta ya habari yaliyoibua vitisho vingi katika
ipatikanaji wa haki za msingi za binaadamu ikiwemo haki ya kupata habari na
kujieleza.
Alisema kwa
kutambua umuhimu wa vyombo vya habari na mabadiliko yanayoikuma sekta hiyo na
wajibu wake kwa jamii ndipo azimio hilo likatolewa ili kuzingatia haja na
mahitaji ya makundi yote ya kijamii.
katika
kupiga vita suala hilo.
Akitoa mada kuhusiana na azimio hilo mkufuzi wa warsha hiyo maalim Juma Ali Simba alisema hali ya
waandishi kuonesha uwajibikaji katika utendaji wa kazi zao ni jambo la lazima kwani bila ya
maadili sekta hiyo haitaweza kufikia lengo la kuwa muhimili wa nne wa
taifa.
Mafunzo hayo ya siku tatu yaliwashirikisha waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali
vya Zanzibar ikiwa ni hatua za Baraza la Habari Tanzania (MCT) katika kuwasilisha rasimu ya azimio hilo la Dar es saalam
lililofikiwa mwaka uliopita.