Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga amemwagiwa tindikakali na watu wasiojulikana asubuhin ya leo wakati akiwa mazoezini huko maeneo ya viwanja vya Mwanakwerekwe, nje kidogo ya manispaa ya mji wa Zanzibar.
Habari zilizopatikana asubuhi hii ni kwamba mara baada ya kutokea kwa tukio hilo, Sheikh alikimbizwa katika hospitali ya Mnazi mmoja ambako alipatiwa huduma ya kwanza kabla ya kusafirishwa kwa ndege ya serikali katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi. Hadi sasa hakuna fununu au watu waliokamatwa au kuhusishwa na tukio hilo.
Pichani, Sheikh Fadhil Soraga akitolewa katika Chumba
cha Huduma ya Mwanzo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kabla ya kusafirishwa kwenda katika hospitali ya muhimbili jijini Dar es salam kwa matibabu zaidi.
|
No comments:
Post a Comment