· BALOZI SEIF AONGOZA VIKAO
· Zapongezwa, wananchi watakiwa kufuatilia taarifa za hali ya hewa
Kamati ya sherehe na maadhimisho ya kitaifa Zanzibar
imekutana kutathmini maadhimisho ya sherehe za miaka 49 ya Mapinduzi ya
Kikao hicho kilichokuwa ya Mwenyekiti wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kilipokea taarifa ya tathmini ya maadhimisho hayo toka kwa kaimu Katibu wa Sekriterieti ya Kamati hiyo ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Said Shaaban ambae alisema kamati zote zilitekeleza vyema majukumu waliyopangiwa.
Said aliwaeleza wajumbe hao kuwa licha ya ufanisi ulioshuhudiwa pia zipo changamoto zilizojichomoza ndani ya utekelezaji wa majukumu ya kamati hizo ambayo ni pamoja na ufinyu wa bajeti kulingana na shughuli zilivyopangwa na ushiriki mdogo wa maafisa wa serikali na masheha kwa dhana ya kuwa sio wahusika.
Alisema katika kufanikisha maadhimisho ya mwakani ambapo Zanzibar
itakuwa inatimiza nusu sekriterieti imependekeza kuvishikisha na kuvitumia ipasavyo vyombo vya habari hasa vya serikali ili kushajiisha umma kuelewa umuhimu wa kushiriki katika maadhimisho.
Aidha Mwenyekiti wa Kamati hiyo alizipongeza kamati zote kwa kufanikisha vyema sherehe hizo na kufahamisha kwamba zilifanikiwa kutokana na ushirikiano mzuri uliokuwepo baina ya viongozi na wafanyakazi wa taasisi za umma, binafsi na wananchi.
“Wakati tunafanya tathmini ya sherehe za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar
tunapaswa kuanza safari kubwa ya sherehe hizi kutimia nusu karne hapo mwakani”. Alisema Balozi Seif.
Nao wajumbe wa kamati hiyo walishukuru ushirikiano waliopatiwa na serikali na kuazimia kukutana tena katika kipindi cha mwezi mmoja ujao ili kupanga mikakati ya maandalizi kwa ajili ya maadhimisho ya mwakani.
Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alikiongoza kikao cha kamati ya Maafa Zanzibar kujadili namna ya taifa linavyoweza kujiandaa dhidi ya maafa au matatizo yoyote yanayoweza kutokea katika kipindi hichi cha mvua za masika zilizokwishaanza.
Kikao hicho kilichojumuisha wajumbe wa kamati hiyo toka Unguja na Pemba kilifanyika katika ukumbi wa Ofisini kwa Makamu huyo wa Rais iliyopo Vuga Mjini Zanzibar .
Akiwasilisha taarifa juu ya mwelekeo wa mvua za masika katika kipindi cha kuanzia mwezi wa Machi hadi Mei, Mkurugenzi wa Idaya ya Maafa Zanzibar Ali Juma Hamad alisema kuwa pamoja matarajio ya mvua kuwa za wastani katika maeneo mengi, bado upo uwezekano wa kutokea miripuko ya magonjwa.
Hamad alisema taasisi zinazohusika na maafa zinapaswa kuchukuwa hatua za tahadhari kufanya maandalizi ya kukabiliana na madhara yanayoweza kusababishwa na mvua za masika.
Akizungumzia sekta ya kilimo na usalama wa chakula Hamad alisema maeneo mengi ya ukanda wa pwani ya kaskazini pamoja na Visiwa vya Zanzibar yanatarajiwa kuwa na unyevu unyevu wa kutosha wa udongo hali ambayo wakulima wanashauriwa kuendelea na taratibu za kawaida za kilimo cha msimu huu wa mvua za masika.
Akikiahirisha Kikao hicho Balozi Iddi aliiagiza Idara hiyo kwa kushirikiana na wataalamu wa taasisi washirika kuandaa utaratibu mahsusi wa kutoa taarifa rasmi kwa wananchi kuanzia wiki ijayo ili kuisaidia jamii kuchukua tahadhari dhidi ya majanga yoyote yanayoweza kutokea katika mvua za masika.
Alisema serikali na wananchi wote wanapaswa kujitayarisha kukabiliana na majanga au maafa ili kuepusha madhara yatakayosababishwa na mvua za masika zilizoanza mapema mwezi huu.
Wakichangia wajumbe wa kamati hiyo walisema wananchi wengi hadi sasa hawajawa na utamaduni ya kufuatilia mienendo ya mifumo ya hali ya hewa nchini ambayo ni muhimu katika maisha yao ya kila siku licha ya taasisi zinazohusika na hali ya hewa kutoa taarifa hizo mara kwa mara.