ASKOFU MUSHI KUZIKWA JUMATANO
MAZISHI ya marehemu Askofu Veratus Gabriel Mushi wa
kanisa katoliki jimbo la zanzibar aliyweuawa kwa kupigwa risasi jana
asubuhi yanatarajia kufanyika Jumatano katika makaburi ya Kitope mkoa wa Kaskazini Unguja.
Akizungungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake Shangani mjini Zanzibar, Askofu Mkuu wa Kanisa hilo
jimbo la Zanzibar Agostino Shao alisema kanisa lake limepokea kwa
mshtuko tukio hilo na kwamba linaendelea na maandalizi ya mazishi
yanayotarajiwa kufanyika katika makaburi ya viongozi wa kanisa hilo
katika kijiji cha Kitope, wilaya ya Kaskazini 'B', Unguja.
Alisema
kanisa lake linafanya mawasiliano na ndugu wa marehemu ili kujua ni
watu gani wataotaka kuhudhuria katika mazishi hayo pamoja na wageni.
"Tunachokifanya
toka jana baada ya kukabidhiwa mwili wa marehemu majira ya saa kumi
jioni ni kuratibu juu ya namna ya mazishi yatakavyokuwa pamoja na wageni
tunaotarajia kuwapokea katika mazishi hayo", alisema Askofu Shao.
Pamoja
na kuelezwa kuridhishwa kwake na hatua zilizochukuliwa na jeshi la
polisi toka kutokea kwa tukio hilo, Askofu Shao alisema ipo haja kwa
jeshi hilo kuhakikisha linawajibika ipasavyo ili kukomesha vitendo vya
uhalifu si tu kwa viongozi wa dini na maeneo yao ya ibada bali pia kwa
raia wote.
Akionesha kutoridhika na kutofanyiwa kazi
kwa taarifa za kutokea kwa matukio mbali mbali dhidi ya kanisa na
viongozi wake, askofu huyo alisema kuna haja maalum kwa Rais kufanya
marekebisho ya uongozi wa jeshi hilo kwa upande wa Zanzibar ili lifanye
kazi kwa kuzingatia sheria na kufanya juhudi katika kuzuia uhalifu kabla
ya kutokea.
"Kuna taarifa nyingi tumekuwa tukitoa kwa
jeshi la polisi lakni taarifa hizi zimekuwa hazifanyiwi kazi kikamilifu
na kuwa ndio chanzo cha matukio mengi ya kihalifu ndani ya nchi",
alisema Askofu Shao.
Monday, February 18, 2013
SMZ YATOA TAMKO
SERIKALI ITWASAKA WALIOMUUA ASKOFU MUSHI
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imewataka wananchi wa imani zote kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili kuviwezesha kufanya uchunguzi wa kifo cha Askofu Varistus Gabriel Mushi kilichotokea jana asubuhi.
Akitoa taarifa ya serikali, Waziri wa nchi Afisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Muhammed Aboud Muhammed ofisini kwake Vuga, alisema serikali italiwezehsa jeshi la polisi na vyombo vyengine ulinzi na usalama ili kubaini chanzo cha matukio hayo yanayoonekana kushamiri siku hadi siku.
Abuod alisema katika wakati huu wa majonzi wananchi na waumini wa dini zote wanapaswa kutulia na kuviacha vyombo hivyo vifanye kazi zao kwa utaalamu na mafunzo yao.
"Serikali haiwezi kuacha matukio kama haya yaendelee kwani yanaibua hofu kwa jamii na kuathiri jina la nchi yetu na uchumi wetu kwa ujumla", alisema Aboud.
Aliongeza kuwa serikali ya Zanzibar inaunga mkono tamko lililotolewa na serikali ya muungano linalovitaka vyombo vya usalama vya ndani na nje ya nchi ili kubaini chanzo cha matukio hayo na kama kuna watu au kundi lolote linalofadhili matukio hayo.
Kuhusu suala la uwezekano wa kuzagaa kwa silaha, Aboud alisema hali hiyo inatokana na mazingira ya Zanzibar yanayowezesha kuwepo kwa bandari zisizo rasmi (bubu) jambo ambalo serikali inalifanyia kazi na kuwataka wananchi kutoa taarifa juu ya watu wanaowatilia shaka kuhusika na vitendo vya uhalifu.
Aidha aliwataka viongozi wa dini kuendelea kuhubiri amani , utulivu na kuvumiliana miongoni mwa waumini wao ili kuiepusha nchi na matatizo ya kijamii na kiuchumi.
"Kwa miaka mingi watu wa dini tofauti wamekuwa wakiishi pamoja kwa mafahamiano na mshikamano hivyo bado kila mmoja wetu anapaswa kutimiza wajibu wake ili kuendeleza mshikamano uliodumu kwa muda mrefu", aliongeza Aboud.
Askofu Mushi aliuawa kwa kupigwa risasi tatu kichwani asubuhi ya Jumapili wakati akienda kuendesha misa ya Jumapili katika kanisa la mtakatifu Theressa liliopo Beit el Ras nje kidogo ya mji wa Zanzibar ambalo ni sehemu ya kanisa Katholiki jimbo kuu la Zanzibar.

Subscribe to:
Posts (Atom)